VIJANA
Saba wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kikosi cha 821 Bulombora wilayani
Uvinza mkoani Kigoma, wamefariki dunia na wengine 22 wamejeruhiwa wengi
wao vibaya baada ya gari walilokuwa wakiafiria kupinduka.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ), Mkoa Kigoma, Kanali Mamdadi Kisui amesema wapiganaji hao
walikutwa na mauti juzi saa 10 jioni katika eneo la Mlima Pasua nje
kidogo ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Kanali
Kisui alisema wapiganaji hao walikuwa wakisafiri na gari la Jeshi aina
ya Iveco lenye namba za usajili 5717 JW 09 lililokuwa likitokea Kambi ya
Burombola, kwenda mjini Kigoma likiwa na vijana 30 wa JKT.
Akijibu
maswali ya waandishi, Kanali Kisui alisema vijana hao ni sehemu ya
vijana waliojiunga na JKT baada ya kuhitimu elimu ya kidato cha sita,
lakini baada ya kumaliza mafunzo ya Jeshi, wakaomba kubakia kambini
wakisubiri taratibu za kujiunga na elimu ya juu.
Naye
mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa Kigoma Maweni, Dk Fadhili Kibaya
alitaja askali waliofariki katika ajali hiyo kuwa Ally Kambagwa, Mkazi
wa Mtwara, Abeli Maisha mkazi wa Morogoro na Eugini Bitati, mkazi wa
Kibondo Mkoani Kigoma.
Wengine
ni pamoja na Saidi Sadara, mkazi wa Kahama mkoani Shinyanga, Bakari
Kibaya mkazi wa Tanga na Fredric Kaemela mkazi wa Njiro mkoani Arusha.
Mganga huyo mfawidhi alitaja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Benedict
Ndokeye, Raphaeli Johanna, Athanasi Emanuel, Abui Nzoge, Abubakari
Peter, Abubakari Msubi, Deusi Manyanya, Edward Nyanda na Eliasi Magesa.
Wengine
ni pamoja na Geofly Maliki, King Kasefu, Kamiliusi Agida, Lameck John,
Martini Kupatu, Stevin Denis, Saidi Omary, Saidi Zuberi, Shabani
Zakaria, Victor Saverxy, Jackson Nyarubu na Muhamed Nyimbo.
Vijana
hao wa JKT waliagwa jana jioni katika Hospitali ya Mkoa Kigoma na
baadaye walisafirishwa kwenda katika mikoa yao kwa maziko ambapo Katibu
Tawala wa Mkoa Kigoma, John Ngunguru aliongoza viongozi wa Serikali na
Kamati ya Ulinzi ya Usalama kuaga na kuwasindikiza akimwakilisha Mkuu wa
Mkoa Kigoma, Issa Machibya ambaye yuko nje ya mkoa kikazi.
Katika
salamu zake kwa niaba ya Serikali, Ndunguru alisema Serikali
imesikitishwa na ajali hiyo na ni pigo kubwa kwao kwani vijana hao
walikuwa nguvu kazi na viongozi wa Taifa katika siku chache zijazo na
wamekutwa na mauti akiwa chuoni wakipikwa kwa ajili ya kulitumikia
Taifa.
Akitoa
salamu kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali
David Mwamunyange, Mkuu wa Jeshi Mkoa Kigoma, Kanali Mamdad Kisui
alisema mkuu wa majeshi amepokea kwa masikitiko makubwa msiba huo
ameungana na ndugu na jamaa katika kuombeleza msiba huo.
|
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.