0
Michuano ya kuwania kufuzu kucheza Euro 2016 imeendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali, moja kati ya mechi zilizochezwa usiku wa October 9, timu ya taifa ya Uingereza ilikuwa mwenyeji wa timu ya taifa ya Estonia.
1444421746643_lc_galleryImage_Football_England_v_Estoni
 Mechi ambayo ilikuwa ngumu kwa Uingereza kuweza kupata nafasi ya kufunga goli kutokana na timu ya taifa ya Estonia kuwa imejiandaa vyema kuwakabili waingereza hao, uwezo wa kuhimiri mashambulizi ya waingereza ulidumu kwa dakika 44 kabla ya dakika ya 45 Theo Walcott kupachika goli la kwanza na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0 dhidi ya Estonia.
1444420076294_lc_galleryImage_SPT_ITE_091015__UEFA_Euro
Uingereza walirudi uwanjani kipindi cha pili wakiwa na faida ya goli moja kitu ambacho kiliwapelekea Estonia kujaribu kutafuta nafasi ya kusawazisha goli hilo ila Raheem Sterling aliwakatisha tamaa ya kusawazisha goli hilo ambalo lingeweza kuwafanya waondoke na Point moja, Sterling alipachika goli la pili dakika ya 85 ya mchezo na kufanya mechi imalizike kwa Uingereza kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
1444416882249_lc_galleryImage_England_s_defender_Nathan
 magoli Uingereza 2-0 Estonia

 magoli ya Hispania 4 – 0 Luxembourg

Matokeo ya mechi nyingine za kuwania Euro 2016 zilizochezwa usiku wa October 9
8

Post a Comment

 
Top