Mahakama nchini Misri imeagiza kuachiliwa huru wa wana wawili wa kiume wa rais aliyeng’olewa mamlakani Hosni Mubarak.
Wawili
hao walikuwa wamefungwa jela miaka mitatu kwa kuhusika katika ufisadi,
shirika la habari linalomilikiwa na serikali Nile News limeripoti.Mahakama iliamuru Alaa na Gamal Mubarak waachiliwe huru baada ya kuzingatia muda ambao wamekaa jela, afisa wa mahakama na wakili wao Farid al-Deeb wameambia shirika la habari la AFP.
Wawili hao walikamatwa na kuzuiliwa mwaka 2011.
Bado wanasubiri uamuzi kuhusu rufani waliyokata dhidi ya hukumu nyingine ya miaka mitatu jela kila mmoja kwa ubadhirifu wa pesa za umma.
Walikuwa pia wanatajwa katika kesi kuhusu kuingilia na kuchezea soko la hisa.
Post a Comment