Serikali
jana ilimfikisha mahakamani bwana Bernedict Angelo Ngonyani kwa tuhuma
za kutumia mtandao wa Facebook na WhatsApp kueneza taarifa za uongo kuwa
mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amelazwa Nairobi
kwa madai ya kulishwa chakula chenye sumu.
Akizungumza
kwenye eneo la mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam ambako mtuhumiwa
huyo alifikishwa kwa ajili ya kusomewa mashitaka, wakili mkuu wa
serikali Joanes Karungura alisema, mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani
hapo kwa kuvunja kifungu namba 16 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya
mwaka 2015.
Sheria
hiyo ijulikanyo kwa lugha ya Kiingereza, Tanzania Cybercrime Act 2015,
inakataza kusambaza ujumbe, taarifa au data za uongo au
zisizothibitishwa kwa njia ya mtandao.
Mhandisi
wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, TCRA anasema watuhumiwa hao walikutwa
na laini zaidi ya mia moja zenye usajili bandia ambazo walikuwa
wanazitumia kufanya biashara ya kupiga simu Kimataifa kinyume cha sheria
Ngonyani
ambaye amenyimwa dhamana kutokana na aina ya kosa alilofanya la kuvunja
sheria ya mtandao ya mwaka 2015 alikamatwa Septemba 25 mwaka huu kwa
ushirikiano wa mamlaka ya mawasiliano nchini, Jeshi la Polisi na vyombo
vya ulinzi na usalama.
Wakati
huo huo serikali imewafikisha watuhumiwa watano katika mahakama ya
Kisutu jijini Dar es Salaam, mmoja raia wa Afrika ya Kusini, mmoja raia
wa China na watatu kutoka Pakstani, kwa kosa la kuiba kwa njia ya
kimtandao wizi wenye thamani ya karibu shilingi billion moja, fedha za
Kitanzania.
Mtuhumiwa
wa makosa ya mtandao Benedict Angelo Ngonyani (24) (wa kwanza kulia)
anayetuhumiwa kusambaza taarifa za uongo zinazomhusu Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama, akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu
akisubiri kusomewa mashitaka.
Wengine ni watuhumiwa wa wizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network) Ally Hamze (53) raia wa Afrika Kusini (wa pili kulia), Huang Kun Bing (26) Raia wa China (wa tatu kulia) Irfan Mirza Baig (46) (wa kwanza kushoto) Hefeez Irfan (32) (wa pili kushoto) na Mirza Rizwan Baig (41) (wa tatu kushoto) wote watatu raia wa Pakistani wakiwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakisubiri kusomewa mashitaka ya wizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network).
Kesi zote zimeahirishwa hadi Oktoba 23 na watuhumiwa wote wamepelekwa rumande huku uchunguzi ukiendelea.
Post a Comment