Watu 150 waliokuwa wakishiriki sherehe za
hija wamefariki kwenye mkanyagano uliotokea
katika mji mtakatifu wa Kiislamu wa Mecca,
maafisa nchini Saudi Arabia wamesema.
Idara ya ulinzi wa raia nchini humo imesema
kupitia Twitter kwamba watu wengine 400
wamejeruhiwa katika kisa hicho kilichotokea
mji wa Mina, takriban kilomita tano kutoka
mji wa Mecca.
Shughuli za uokoaji zinaendelea, idara hiyo
imeongeza.
Mkanyagano huo umetokea siku ya kwanza ya
sherehe za Eid al-Adha.bbc
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment