0

Mamia ya wakimbizi walio na nia
ya kuondoka nchini Hungary
wameanza kuvuka mpaka kwenda
nchini Austria ambapo
wamepokewa katika kituo kimoja
cha muda cha shirika la msalaba
mwekundu wakionekana
wamechoka lakini wakiwa na
furaha.
Mabasi ya Hungary yaliwafikisha
mpakani ambapo walitembea na
kuingia nchini Austria.
Msemaji wa polisi nchini Austria
( Werner Fasching) alisema kuwa
karibu watu 3000 wanatarajiwa
kuwasili saa chache zinazokuja.
Austria inasema kuwa wakimbizi
hao wanaweza kuomba hifadhi
nchini humo au waendelee na
safari yao kwenda nchini
Ujerumani ikiwa watapenda hivyo

Post a Comment

 
Top