0

Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini
humo zifungwe kuanzia Jumatatu huku
mgomo wa walimu ukiendelea.
Barua kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza
shule zote za umma na za kibinafsi zifungwe
na wanafunzi warudi nyumbani.
Watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi
wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya
darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.
Katibu Mkuu wa chama cha walimu nchini
humo KNUT ameambia BBC kuwa tayari
amepokea barua hiyo ya kufungwa kwa shule
kutoka kwa serikali.
Amesema chama hicho kilikuwa kimeishauri
serikali ifunge shule “zamani”.
Mahakama inatarajiwa kuamua Ijumaa ijayo
iwapo mgomo huo wa walimu, ambao
umelemaza masomo muhula wa tatu, ni halali
au la.

Post a Comment

 
Top