Rais wa mpito wa Burkina Faso Michel
Kafando aliyeondolewa mamlakani na kikosi
cha walinzi wa rais ameachiliwa huru na yuko
buheri wa afya, viongozi wa mapinduzi
wamesema.
Hata hivyo, Waziri Mkuu Isaac Zida,
aliyezuiliwa wakati mmoja na walinzi hao
walipovamia mkutano wa baraza la mawaziri,
amewekwa kwenye kizuizi cha nyumbani.
Viongozi hao wa mapinduzi wamekubaliana
kuhusu mambo muhimu ya kujadiliwa, huku
marais wawili wa mataifa ya Afrika Kusini
wakiwasili nchini humo kuongoza
mashauriano.
Rais Macky Sall wa Senegal na Thomas Boni
Yayi wa Benin, walielekea Burkina Faso
kufanya mashauriano na viongozi waliopindua
serikali.
Rafiki wa karibu wa kiongozi wa zamani
Blaise Compaore anayeishi uhamishoni Ivory
Coast, Jenerali Gilbert Diendere, alitangazwa
kiongozi mpya na walinzi hao Alhamisi.
Viongozi wa Amerika, Ufaransa na Muungano
wa Afrika (AU) wameshutumu mapinduzi
hayo.
Watu watatu wanadaiwa kuuawa baada ya
wanajeshi wa kikosi hicho cha walinzi
maalum wa rais (RSP) kuwakabili
waandamanaji katika jiji kuu la Ouagadougou.
Shirika la kijamii lenye ushawishi mkubwa la
Balai Citoyen limesema waliouawa ni 10.
Idadi isiyojulikana ya waandamanaji
wanaopinga mapinduzi hayo pia
wamekamatwa na kuzuiliwa.
Viongozi hao wa mapinduzi wametangaza
amri ya kutotoka nje usiku nchini humo na
kufunga mipaka yote ya taifa hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment