UWANJA
wa Azam ambao ndiyo wa kisasa baada ya ule wa Taifa, Dar es Salaam
ulijengwa kwa Sh 2 bilioni za Kitanzania hadi kuanza kutumika kwa mechi
za Ligi Kuu Bara.
Lakini
katika hali ya kushangaza Straika wa Taifa Stars, Mbwana Samatta
amegomea kiasi kama hicho cha fedha kujiunga na Zamalek ya Misri.
Katika
kuonyesha jeuri zaidi, Samatta amesema pia hataongeza mkataba na klabu
yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hata kama bosi
wa timu hiyo Moise Katumbi atampa dau la maana kwa kuwa ndoto zake si
kuendelea kucheza Afrika.
Samatta
alisema ndoto zake kwa sasa ni kucheza soka la kulipwa Barani Ulaya na
hawezi kuongeza mkataba wa kuichezea Mazembe, huku pia akikiri kuligomea
dili la Zamalek ambalo lingempa Sh 2 bilioni.
Nyota
huyo wa zamani wa Simba alikiri kuwa jitihada zake za kutimkia Ulaya
mwaka huu tayari zimegonga mwamba, lakini hajakata tamaa na hataongeza
mkataba Mazembe ili kujiongezea nafasi ya kujiunga na klabu za Ulaya.
“Dirisha
limefungwa tayari kwa sasa, ila sijakata tamaa, nasubiri tena dirisha
lijalo, mkataba wangu pia utakuwa unamalizika hivyo nitakuwa na nafasi
kubwa zaidi,” alisema Samatta
“Kuhusu
kuongeza mkataba Mazembe hapana, sina mpango huo, sina ndoto za kucheza
tena Afrika na ndiyo sababu nilikataa dili la Zamalek hivi majuzi,
sikupenda kujiunga nayo maana siyo ndoto yangu,” aliongeza.
Chanzo:Mwanaspoti
Post a Comment