0

Maelfu ya wazazi na wanafunzi wamejitokeza
kumuunga mkono mwanafunzi mmoja shupavu
aliyepata sufuri katika mtihani wake wote wa
mwisho.
Amini usiamini,Mariam Malaka ambaye
amekuwa mwanafunzi wa kupigiwa mfano
nchini Misri kutokana na alama za juu
alizopata katika mitihani ya awali, alikuwa na
matarajio ya kuzoa alama ya juu zaidi yaani
A itakayomwezesha kujiunga na chuo cha
mafunzo ya daktari lakini wapi ?
Katika mtihani wake wa mwisho Mariam
Malak alipewa alama za chini zaidi .
Hii ikimaanisha kuwa, bi Malak hakuandika
hata herufi moja aliyojibu kikamilifu.
Bi Mariam Malak anashuku kuwa kulitokea
kosa kubwa kwani yeye alivyofanya mtihani
huo hadhani kama angeufeli.
''Kwa kweli sikuamini macho yangu eti
nimefeli mtihani wa mwisho'' bi Mariam Malak
aliiambia BBC.
Alizimia alipotafuta jina lake na akaikosa
katika orodha ya watahiniwa waliopasi
mtihani wao wa mwisho.
Malak alikuwa hajaufeli mtihani mmoja bali
alikuwa amezoa sufuri katika masomo yote
saba.
Yaani alikuwa ameambulia sufuri juu ya mia
0% katika masomo yote saba.
''Hii sio kweli''
Familia yake inadai kuwa huwenda malak
ameangushwa mtihani wake wa mwisho
maksudi tu kwa sababu ya hila.
Awali ilidhaniwa kuwa alichukiwa kwa sababu
yeye ni wa kutoka kwenye tabaka la Wamisri
wachache ambao ni wakristo wa kicoptic
lakini dhana hio ilikataliwa.
Familia yake inahofia huenda hii ikawa ni
njama ya kumpokonya mwanawao ndoto yake
ya kuwa daktari.
Wizara ya Elimu imelazimika kumpa mtihani
wa kubaini iwapo hati iliyowakilishwa kwa jina
lake ni yake haswa ama ni ghushi, hata hivyo
ikatoa uamuzi kuwa ilikuwa yake haswa.
Hata hivyo maelfu ya watu waliotazama
nakala za hati aliyoandika kwenye runinga
walisema hazifanani kabisa na zile zilizopewa
jina lake.
Kufuatia tofauti hiyo, ukurasa ulianzishwa
kwa nia ya kuishinikiza wizara ya elimu
kuingilia kati kutanzua kitendawaili hicho.
Ukurasa huo unawafuasi takriban 30,000
kufikia sasa.
Tayari watu kadha wamejitokeza kugharamia
malipo yake yote ya chuo kikuu.
Ndugu yake Mina anasema kuwa wanashuku
majibu yake yalipewa mtu mwengine.

Post a Comment

 
Top