0

Tanzania imeisimamisha Malawi isiteketeze
moto tani 2.6 ya pembe ya ndovu ilizonasa
katika operesheni dhidi ya wawindaji haramu
Shehena hiyo ya meno 800 ya ndovu ilinaswa
na maafisa wa forodha wa Malawi ilipokuwa
ikiingizwa nchini Malawi.
Tanzania ilikimbia mahakamani ilikuizuia
serikali ya Malawi isiharibu ushahidi wake
dhidi ya watuhumiwa waliokamatwa na kesi
inaendelea.
Mkurugenzi mkuu wa idara ya kuwalinda
wanyama pori wa Malawi anasema kuwa
inasikitisha mno kuwa Tanzania imekwenda
mahakamani kuizuia idara yake isiteketeza
bidhaa hizo haramu kwa miezi mitatu ijayo.
''Tulikuwa tayari kuchoma moto pembe hizo
za ndovu ambayo ingekuwa ishara kamili
kuwa tunapanga mikakati kabambe ya
kupambana na walanguzi na wawindaji
haramu ili kulinda ndovu wetu,''
''Sasa hilo halitawezekana kwa sasa na hadi
baada ya miezi mitatu ijayo'' alifoka Bright
Kumchedwa
Idadi ya ndovu imepungua kwa asilimia 50%
tangu mwaka wa 1980 nchini Malawi
kutokana na uwindaji haramu.
Nchini Tanzania Idadi ya ndovu imepungua
kwa asilimia 60% katika kipindi cha miaka
mitano tu iliyopita.
Mwezi uliopita mahakama moja iliwapata na
hatia kaka wawili raia wa Malawi na hatia ya
uwindaji haramu na ulanguzi wa pembe za
ndovu.
Wawili hao walipigwa faini ya dola elfu tano
za Marekani $5,500 na mahakama ikaamuru
bidhaa hiyo ichomwe moto katika kipindi cha
siku 20.
Lakini serikali ya Tanzania nayo ikakimbia
mahakamani ilikuzuia serikali ya Malawi
isiteketeza pembe hizo ikidai kuwa itakosa
ushahidi wowote dhidi ya watuhumiwa wake
wa uwindaji haramu.
Tatizo la uwindaji haramu umekithiri katika
miaka ya hivi karibuni kufuatia utashi
mkubwa wa bidhaa hiyo inayoenzia katika
mataifa ya mashariki ya mbali na bara Asia.
Si aghalabu kushuhudia familia nzima ya
ndovu na faru wakiangamizwa katika mbuga
za wanyama pori barani Afrika ambako ndovu
bado wapo.
Mwaka uliopita viongozi wa mataifa ya
Botswana, Gabon, Chad na Tanzania
yaliafikiana kuthibiti uuzaji wa pembe za
ndovu.bbc

Post a Comment

 
Top