Neymar
Mshambuliaji wa
Barcelona Neymar amethibitisha kuwa alikuwa na mazungumzo kuhusu
kujiunga na Manchester United msimu huu lakini hakupokea ombi thabiti.
United ilihusishwa na uhamisho wa raia huyo wa Brazil,aliyefunga mabao 57 ya Barcelona mwishoni mwa dirisha la uhamisho.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amesema kuwa:''Kulikuwa na mazungumzo lakini hakukuwepo na majadiliano ya kina''.
Naibu mwenyekiti wa kilabu ya Manchester United Ed Woodward alielekea Barcelona mwezi uliopita alipojaribu kufanikisha uhamisho wa Pedro ambaye baadaye alijiunga na Chelsea.
Post a Comment