Kafando
Serikali ya
Burkina Faso imevunja kikosa cha kumlinda rais ambacho kiliwashika
mateka mawaziri wakati wa majaribio ya mapinduzi yaliyofeli.
Hatua
hiyo ilichukuliwa wakati wa mkutano wa kwanza wa serikali tangu siku ya
Jumatano wakati rais wa mpito Michel Kafando aliporejeea madarakani.Waziri wa masuala ya ulinzi amefutwa kazi na tume imebuniwa kuwatambua wale waliohusika katika kupanga mapinduzi hayo.
Takriban watu 19 waliuawa wakati wa maandamano ya kupinga mapinduzi hayo.
Post a Comment