MGOMBEA wa nafasi ya ubunge kupitia
chama cha mapinduzi jimbo la Masasi
Rashid Chuachua amewaomba wanachama
na wananchi wa jimbo hilo kumchagua ili
aweze kuboresha sekta ya kilimo kwa
kurasimisha ardhi ya wakulima waweze
kupata hati za kimila zitakazowawezesha
kupata mikopo kwenye taasisi za kifedha
nchini.
Pia ametoa matumaini mapya kwa
wafanyakazi wa sekta ya umma hususani
walimu kwa kuwaahidi kuwa endapo
watamchagua na kuwa mbunge wa jimbo
hilo atahakikisha wanalipwa stahili zao
ikiwemo malimbikizo ya mishahara kwa wale
walimu waliopanda madaraja sambamba na
kutoa mafunzo kazini kwa walimu hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment