Wananchi wa jimbo la Liwale mkoani Lindi waliamua kukesha kwenye uwanja wa mpira kumsubili mgombea urais kupitia vyama vinavyounda UKAWA,Edwardi Lowassa mpaka alipowasili majira ya saa 9 alhasili walitimiza saa 19 kwa kile wanachotaka Mabadiliko.
Sumaye alisema imefika wakati wa wananchi kuhitaji kufaidi matunda ya mfumo wa vyama vingi kwa kutaka Mabadiliko ndani ya vyama vya upinzani ambapo ccm imeshindwa kusimamia na imekuwa kuburi kwakuwa imetawala muda mrefu na kushindwa kutatua matatizo na amewambia kama mutaendelea kuichagua ccm maisha yataendelea kuwa magumu siku zote.
Lowassa awatoa wasiwasi wananchi wa jimbo la Liwale mkoani Lindi kwa matokeo ya utafiti uliotolewa hivi karibuni na amesema kura kamili zitajulikana octoba 25 hivyo amewaomba wapiga kura kumchagua yeye kwa kura za kutosha zitakazo mwezesha kutangazwa mshindi wa kiti cha urais.
Pia awahaidi wakazi wa Liwale akipta ridhaa ya kuchaguliwa elimu kuanzia chekechea hadi Chuo kikuu itakuwa bure,kilimo atakiboresha na kitakuwa cha kisasa na pia ahaidi mfumo wa stabadhi ghalani ataupa siku 10 kama utakuwa kandamizi atauondoa na kuwa soko uria.
Mgombea ubunge kupitia Chama cha CUF,Zuberi kuchauka akiomba kupigiwa kura na wapiga kura mbele ya mgombea urais alisema akichaguliwa atatatua kero zinazo ikumba Jimbo la Liwale ikiwe barabara ya Liwale kuunganisha na barabara ya Nangurukuru kwa kiwango cha rami kwani wananchi wa Liwale ndio barabara wanayoitumia kwa kila siku kusafirisha mazao na kutumika kusafirisha bidhaa za wafanyabiashara.
Kuchauka aliongeza kusema Liwale inahitaji kufunguliwa kwa barabara zinazounganisha Liwale na mikoa ya Morogoro na Ruvuma kama barabara hizi zitafunguliwa itakuwa inaleta tija kwa wanaliwale.
Post a Comment