Boti iliyojaa wahamiaji
imezama karibu na
pwani ya Libya, na
inahofiwa kwamba
watu 200 wamekufa
katika ajali hiyo. Na
Austria imesema idadi
ya maiti za wahamiaji
zilizokutwa nchini
humo, imepindukia 70.
Afisa wa usalama
katika mji wa Zuwara
magharibi mwa Libya
ambako boti hiyo
iliyozama ilianzia
safari yake, amesema
iling'oa nanga ikiwa na
watu zaidi ya 400
ndani yake.
Afisa huyo ameendelea
kueleza kwamba hadi
jana jioni walinzi wa
mwambao wa Libya
walikuwa
wamefanikiwa
kuwaokoa watu 201,
na 147 miongoni mwao
walipelekwa moja kwa
moja kwenye kizuizi
kwa ajili ya wahamiaji
haramu, kilicho
Sabratha magharibi
mwa mji mkuu,
Tripoli.
Wasema
wamelazimika
kuchukua njia
hiyo
Wengi wa wahamiaji
waliokuwa wakisafiri
na boti hiyo wanatoka
katika nchi za Afrika
Kusini ya jangwa la
Sahara, Pakistan, Syria
na Morocco. Mmoja wa
wahamiaji
walionusurika ajali
hiyo, Ayman Tallaal
kutoka Syria
amewashukuru
waliomuokoa.
Amesema,
''Tumelazimika
kuifuata njia hii,
ambayo inaitwa njia ya
kifo, na sasa inaitwa
kaburi la bahari ya
Mediterania. Boti
ilikuwa katika hali
mbaya, na watu wetu
wamekufa. Walibya
wametuokoa, Mungu
awabariki''.
Msemaji wa shirika la
msaada la Hialali
nyekundu, Khamis bin
Omar, amesema hadi
jana watu 66 walikuwa
wamethibitishwa
kufariki.
''Leo hii tumepata
taarifa taarifa kuhusu
ajali ya boti ya
wahamiaji kwenye
ufuo wa mji wa
Zuwara. Timu yetu
imewaokoa watu 198
ambao wanatoka
mataifa mbali mbali.
Watu 66, pia kutoka
nchi mbali mbali,
wamekufa hadi sasa''.
Amesema Omar.
Libya uchochoro
Libya imekuwa njia
muhimu inayotumiwa
na wasafirishaji
haramu wa binadamu,
wanaoapeleka
wahamiaji nchini
Italia. Walinzi wa
pwani ya nchi hiyo
wana vifaa duni, na
hutegemea boti za
kujazwa hewa, na meli
za uvuvi.
Shirika la Kimataifa
linaloshughulikia
wahamiaji, IOM
limesema watu 2,300
wamezama katika
bahari ya Mediterania
mwaka huu, na mwaka
jana wengine 3,279
walikufa katika bahari
hiyo wakijaribu
kuvuka kwenda Ulaya.
Maiti 70 ndani ya
lori Austria
Wakati huo huo,
wizara ya mambo ya
ndani ya Austria
imesema leo kuwa
idadi ya maiti
zilizopatikana katika
lori lililotelekezwa
kwenye barabara kuu
nchini humo
imepindukia 70.
Kansela wa Ujerumani
Angela Merkel ambaye
yuko nchini Austria
kuhudhuria mkutano
wa Umoja wa Ulaya
kuhusu mzozo wa
wahamiaji, amesema
ameshtushwa na
taarifa za mkasa huo
wa wahamiaji, na
kusema anayo
matumaini Ulaya
itaushughulikia kwa
pamoja mzozo huu wa
wahamiaji unaozidi
kupamba moto.
Bado yapo maswali
mengi yasio na majibu
kuhusu kisa hicho cha
maiti za wahamiaji
zilizokutwa ndani ya
lori, kama wapi
walikotoka wahamiaji
hao, na nani aliyekuwa
akiwasafirisha.
Wakaguzi wa barabara
walilikuta barabarani
lori hilo likiwa
limetelekezwa, likiwa
na nembo ya kampuni
ya ufugaji wa kuku ya
Slovakia, na nambari
za usajili za Hungary.
Tarifa za hivi karibuni
zimeeleza kuwa
Austria imewatia
mbaroni watu watatu
kuhusiana na kisa
hicho.DW
Post a Comment