Mamia ya vijana wilayani
Masasi jana waliandamana
hadi ofisi za chama cha Wananchi
CUF wilayani Masasi wakipinga
maamuzi ya UKAWA ya
kumsimamisha mwenyekiti wa
NLD Taifa Dkt.Emanuel Makaidi
kuwa mgombea wa ubunge katka jimbo
la Masasi na kwamba wao
wanayemtaka ni Ismail Makombe
(Kundambanda) anayewania
nafasi hiyo kupitia CUF kwa kile walichodai Kundambanda ndio aliyekubalika na watu wengi na huku
wakiapa mbele ya mwenyekiti wa
CUF wilaya ya Masasi Selemani
Matola kuwa endapo UKAWA
wataendelea na mpango huo basi
wao watampigia kura mgombea
wa CCM mwalimu Rashid.
Baadhi ya wafuasi waliokusanyika walipoongea na vyombo vya habari walisema wanataka kundambanda hata kama hana ELIMU ya juu ila yeye ndio kipenzi cha watu wengi kama Lowassa.
Masasi jana waliandamana
hadi ofisi za chama cha Wananchi
CUF wilayani Masasi wakipinga
maamuzi ya UKAWA ya
kumsimamisha mwenyekiti wa
NLD Taifa Dkt.Emanuel Makaidi
kuwa mgombea wa ubunge katka jimbo
la Masasi na kwamba wao
wanayemtaka ni Ismail Makombe
(Kundambanda) anayewania
nafasi hiyo kupitia CUF kwa kile walichodai Kundambanda ndio aliyekubalika na watu wengi na huku
wakiapa mbele ya mwenyekiti wa
CUF wilaya ya Masasi Selemani
Matola kuwa endapo UKAWA
wataendelea na mpango huo basi
wao watampigia kura mgombea
wa CCM mwalimu Rashid.
Baadhi ya wafuasi waliokusanyika walipoongea na vyombo vya habari walisema wanataka kundambanda hata kama hana ELIMU ya juu ila yeye ndio kipenzi cha watu wengi kama Lowassa.
Kundambanda alipopigiwa simu alisema yeye yupo Newala mkoani Mtwara na hana taarifa ya maandamano hayo na aliongeza kusema uhamuzi wa Ukawa kwa ngazi ya juu wapo sahihi kumsimamisha mgombea wa NLD bwana Makaidi lakini hawakufuata utaratibu wa kuangalia matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2014 na hawakufanya utafiti kama nani aliyekubalika zaidi katika jimbo la Masasi.
Aidha katika mgawanyo huo,kwa mkoa wa mtwara
majimbo yaligawanywa kama ifuatavyo.Newala Mjini,CUF..Newala Vijijini
CUF..,Tandahimba CUF..,Mtwara Vijijini CUF,Nanyumbu CUF, Lulindi NLD,Masasi
NLD,Ndanda NLD
Post a Comment