Afisa mmoja wa polisi ameuawa
na wengine zaidi ya mia moja
kujeruhiwa nje ya jengo la bunge
la Ukraine, baada ya wabunge wa
nchi hiyo kuunga mkono mpango
wa awali wa kuipa eneo
linalothibitiwa na waasi Mashariki
mwa nchi hiyo, mamlaka ya
kijitawala.
Waandamanaji waliwarushia
mawe na mabomu ya petroli
maafisa hao na kuna ripoti kuwa
kulitokea mlipuko kati kati mwa
waandamanaji hao.
Maandamano hayo yalitokea
muda mfupi baada ya wabunge
kuidhinisha eneo la Donetsk na
Luhansk ambayo yamo chini ya
waasi wanaoungwa mkono na
Urussi mamlaka zaidi.
Mkataba wa amani wa kusitisha
mapigano ungali unadumisha
nchini humo.
Mkataba wa amani wavunjwa
Mpango huo ulioidhinishwa na
wabunge na sehemu ya mkataba
huo uliosainiwa mwezi Februari
mjini Minsk.
Wakati huu wa msimu wa joto
mapigano kati ya wanajeshi wa
Ukraine na waasi yameongezeka.
Lakini pande hizo mbili
ziliafikiana wiki iliyopita kusitisha
mapigano hayo hiyo kesho,
wakati wanafunzi watakapokuwa
wakirejea shuleni.
Licha ya kuwa mikataba kadhaa
ya kusitisha mapigano
yamekiukwa katika siku za hivi
karibuni, afisa mmoja
mwandamizi wa shirika la
kimataifa la OSCE, nchini Ukraine,
Alexander Hug, ameonya kuwa
hakuna upande wowote katika
mzozo huo umedumisha mkataba
huo wa kusitishwa mapigano.
Lakini muda mfupi baada ya
wabunge 265, kuidhisha mswada
huo wa ugatuzi katika bunge la
nchi hiyo, maandamano nje ya
bunge yakachacha.
na wengine zaidi ya mia moja
kujeruhiwa nje ya jengo la bunge
la Ukraine, baada ya wabunge wa
nchi hiyo kuunga mkono mpango
wa awali wa kuipa eneo
linalothibitiwa na waasi Mashariki
mwa nchi hiyo, mamlaka ya
kijitawala.
Waandamanaji waliwarushia
mawe na mabomu ya petroli
maafisa hao na kuna ripoti kuwa
kulitokea mlipuko kati kati mwa
waandamanaji hao.
Maandamano hayo yalitokea
muda mfupi baada ya wabunge
kuidhinisha eneo la Donetsk na
Luhansk ambayo yamo chini ya
waasi wanaoungwa mkono na
Urussi mamlaka zaidi.
Mkataba wa amani wa kusitisha
mapigano ungali unadumisha
nchini humo.
Mkataba wa amani wavunjwa
Mpango huo ulioidhinishwa na
wabunge na sehemu ya mkataba
huo uliosainiwa mwezi Februari
mjini Minsk.
Wakati huu wa msimu wa joto
mapigano kati ya wanajeshi wa
Ukraine na waasi yameongezeka.
Lakini pande hizo mbili
ziliafikiana wiki iliyopita kusitisha
mapigano hayo hiyo kesho,
wakati wanafunzi watakapokuwa
wakirejea shuleni.
Licha ya kuwa mikataba kadhaa
ya kusitisha mapigano
yamekiukwa katika siku za hivi
karibuni, afisa mmoja
mwandamizi wa shirika la
kimataifa la OSCE, nchini Ukraine,
Alexander Hug, ameonya kuwa
hakuna upande wowote katika
mzozo huo umedumisha mkataba
huo wa kusitishwa mapigano.
Lakini muda mfupi baada ya
wabunge 265, kuidhisha mswada
huo wa ugatuzi katika bunge la
nchi hiyo, maandamano nje ya
bunge yakachacha.
Post a Comment