0


Mechi ya kirafiki baina ya Mbeya City FC dhidi ya mabingwa wa kabumbu Tanzania bara, Dar es salaam Young Africans tayari imeanza kuteka hisia za mashabiki wa soka jijini Mbeya.
Mchezo huo utakaopigwa Jumapili ya wiki hii uwanja wa sokoine Mbeya  utaanza majira ya saa 10:00 jioni.
Wenyeji wa mtanange huo wametangaza kiingilio kuwa ni Shilingi 40,00/=
Mbeya City haijawahi kuifunga Yanga katika mechi mbili walizokutana uwanja wa Sokoine.
Msimu wa mwaka juzi, City wakiwa katika ubora wa hali ya juu walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Yanga na msimu uliopita walikufa 3-1.
Uwanja wa Taifa Dar es salaam, pia Mbeya City haijawahi kuifunga Yanga kwani mechi ya kwanza msimu wa 2013/2014, Wanajangwani walishinda 1-0 na msimu uliopita walikinyuka 3-1 kikosi hicho cha Juma Mwambusi .
Kwa maana hiyo, Yanga imeshindikana mbele ya Wagonga nyundo wa Mbeya.
Je, watapindu rekodi hii Jumapili?

Post a Comment

 
Top