Mwaandishi wetu Kilwa
Wananchi wa kata ya Mitole wilayani Kilwa mkoani Lindi wameiomba
serikali chakula cha msaada ili kukabiliana
baa la njaa linalowakabili lilosababisha na ukosefu wa mvua.
Ombi hilo liletolewa na wananchi hao wakati walipokuwa
wanazungumza na timu ya waandishi wa
habari waliotembelea kijiji hapo.
Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa kijiji hicho Haji
Katumbusi alisema wananchi wameanza
kwenda porini kutafuta matunda na mizizi (Angadi)kwa ajili ya chakula ili
kukabiliana na hali hiyo.
Katumbusi alisema kuwa katika kijiji chao kuna hali mbaya ya
ukosefu wa chakula jambo ambalo uwalazimu kwenda kutafuta matunda na mizizi ya porini ili kujikimu.
“Hali kwa kweli ni mbaya kwani wananchi wanatumia muda mwingi na kutembea umbali
mrefu kutafuta matunda ya pori, mizizi ili iweze kuokoa maisha ya watoto baada ya kutumika kama chakula” alisema
Katumbusi
Nae Diwani wa kata ya Mitole wilayani Kilwa Rafii Kuchao
alikiri kuwepo kwa tatizo hilo la njaa
na kuiomba serikali kupeleka chakula cha bei nafuu haraka na cha
kutosha ili kiweze kuokoa maisha
ya wananchi wa kata hiyo.
“Wanawake na watoto ndiyo wanaodhirika sana na tatizo ili la njaa kutokana na kundi hili
kutoweza kukimbia kutoka nje ya kijiji na maeneo menginen kwa lengo la
kujisalimisha” alisema Kuchao
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Kilwa Abdala Ulega alisema tayari
ofisi yake imetoa taarifa kwa mkuu wa
mkoa Lindi na limefanyiwa kazi kwani mpaka sasa tani
200 za mahindi zimeshafika ambazo zitapelekwa maeneo na vijiji 84 wilayani humo vilivyokubwa
na tatizo la njaa
Post a Comment