Utawala nchini Somalia umeviamrisha vyombo vya habari nchini humo kulipa kundi la wanamgambo wa Al Shaabab jina jipya.
Serikali ya Somalia inataka Al Shaabab kupewa jina la kundi linalowaua watu wa Somalia.Mkuu wa kitengo cha kitaifa cha ujasusi nchini Somalia (Abdirahman Mohamud Tur-yare) anasema kuwa jina Al Shabaab ambalo humaanisha vijana, haliwezi kuhusishwa na wanamgambo.
Alisema kuwa kundi hilo linastahili jina hilo kwa kuwa linaendelea kuwaua watu zaidi.
Nalo likijibu amri hiyo,Alshabaab limesema kuwa raia wa Somalia wanafaa kuiita serikali ya Somalia kama inayowafedhehesha raia wake.BBC
Post a Comment