NkurunzizaRais Jakaya Kikwete wa Tanzania ambaye kwa sasa ni mwenyekiti
wa Jumuia ya Afrika Mashariki amewataka mawaziri wa mambo ya nje kutoka
nchi wanachama kufanya mazungumzo nchini Burundi, Jumatano kabla ya
mkutano wa viongozi wa jumuia hiyo.
Mindi Kasiga mkuu wa kitengo
cha mawasiliano kwa umma katika wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa
kimataifa nchini Tanzania na kusema mazungumzo hayo yanatarajiwa kuwa
ya kwanza kufanyika kuelekea kikao cha dharura cha wakuu wa nchi za
Jumuia ya Afrika Mashariki.Hii ni mara ya kwanza kwa jumuia hiyo kutuma ujumbe wa ngazi ya mawaziri kwenda Bujumbura katika jitihada za kujaribu kumaliza mgogoro wa kisiasa katika nchi hiyo ambayo kwa miaka mingi imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Hatua hiyo imekuja wakati ambapo viongozi wamekosolewa kwa kukaa kimya huku hali nchini Burundi ikizidi kuzorota.
Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Laurent Kavakure alikuwa nchini Tanzania jana Jumatatu ambako alifanya mazungumzo na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe kabla ya kutolewa kwa taarifa hiyo.
Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Burundi kimesema watu wapatao kumi na wawili wameuawa tangu maandamano kuanza tarehe 26 Aprili baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuteuliwa na chama chake tawala cha CNDD-FDD kugombea katika uchaguzi wa Juni mwaka huu.BBC
Post a Comment