Add caption
PICHANI NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRSIA NA MAENDELEO FREEMAN BOWE AKIZUNGUMZA NA MADEREVA MBALIMBALI UBUNGO LEO
Mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA mh FREMAN MBOWE
amewasili leo katika stend ya mabas ubungo kuzungumza na madereva ambao
walikuwa wakiendeah mgomo wa kuwataka serikali iwasikilize shida zao.mh
Mbowe ambaye aliwasili hapa majira ya saa nne kasoroo asubuhi alijikuta
katika wakati mgumu baada ya wananchi kumshangilia kwa nguvu huku
wengine wakifuta barabara ili gari yake ipite huku nyimbo zza ukawa
zikiimbwa,jambo ambalo lilizua taharuki katika eneo hilo.Mh mbowe
alipata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa madereva hao.aidha viongozi
kadhaa wa serikali waliokuwa katika eneo hilo walionekana kuzomewa na
kutokuaminika na madereva hao.
Kuhusu mgomo huo Mkuu wa wilaya ya kinondoni mh PAUL MAKONDA amewaomba
madereva hao kuendelea na kazi na ndani ya siku saba serikali itakua
tayari imeshatoa tamko.
Madereva hao wamekubali kuanza safari kwa sharti la ndani ya siku saba
wawe wamesikilizwa kero zao.MH MBOWE alipotaka kuzngumza na madereva hao
microfone zote zilizimwa na kufichwa kusikojulikana jambo ambalo
lilifanya ashindwe kusikika kwa madereva hao na kuamua kumtoa nje na
kusukuma gari yake hadi maeneo ya shekilango na kurudi opfisini.Taarifa
ni kuwa mgomo huo umekwishwa na magari hapa ubungo yameanza kutoka.
Post a Comment