Na mwaandishi wetu NACHINGWEA
,Ufinyu wa fedha za ruzuku ya uendeshaji wa shule za msingi na sekondari(Capitation Grant) umelalamikiwa kuwa unachangia kwa kiasi kikubwa kudidimiza elimu, kuathiri utoaji wa taaluma na kuwabebesha mzingo wazazi na walezi na kutofikiwa matokeo makubwa sasa (BRN)katika wilaya ya Nachingwea.
Wakizungumza wakati wa maadhimisho ya kilele cha juma la elimu yaliyofanyika siku ya ijumaa(iliyopita) wilayani hapa, baadhi ya walimu wakuu na wakuu wa shulena wazazi waliiomba serikali kupeleka fedha hizo kadiri ya mahitaji ya shule na kwa wakati.
Carlos Matuta,mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Majengo ,alisema kuwa changamoto kubwa inatokana na ufinyu wa fedha hizo zinazotolewa kuwa chache ikilinganishwa na kiasi kinachoidhinishwa katika bajeti.
Alibainisha kuwa kutokana na hali hiyo inawalazimu kuwaomba wazazi na walezi kuchangia michango mbalimbali ili kuziba mapungufu katika uendeshaji wa shule hata hivyo kasi ya uchangiaji ni ndogo kutokana na mwamko mdogo wa jamii katika sual la elimu.
Frola Athuman Millanzi, mwalimu wa shule ya msingi ya Nachingwea alisema kuwa ufinyu wa fedha za kuendeshea shule unachangia utoro kwa wanafunzi ambao wazazi na walezi hawana uwezo wa kifedha hivyo kuiomba serikali kuhakikisha inatoa kiwango kinachotakiwa tena kwa wakati.
Alisema kuwa licha ya ufinyu pia fedha hizo zinachelewa kupelekwa kwenye shule husika hivyo kuwapa mzingo wakuu wa shule na walimu wakuu katika kuendesha shule na kufikia wakati kulazimika kutumia fedha zao za mishahara kuendesha shule .
Delfina Chikawe akizungumza kwaniaba ya wazazi aliitaka serikali kama haina uwezo wa kutoa hiyo ruzuku hiyo kuiondoa ili wazazi wajue kuwa jukumu hilo lipo kwako kuliko mtindo wa sasa ambapo wanadai serikali inagharamia kumbe mzingo ni wao.
Alisema kuwa wazazi kwa sasa wanakabiliwa na michango ambayo haiwashirikishi tena mikubwa na kuomba serikali iwapo inashindwa kugharamia elimu hivi sasa wakati ambapo kwa shule ya sekondari kuna ada kidogo je hapo mwakani ambapo elimu itakuwa bure hali itakuwaje.
Kwa upande wake afisa elimu msingi wa halmashauri ya Nachingwea,Makwasa Bulenga kwenye taarifa ya hali ya elimu aliyoisoma kwenye maadhimisho hayo alitja changamoto fedha za uendeshaji ambapo alisema zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka.
Bulenga alitoa takwimu ambazo zinaonesha kuwa fedha hizo kwa miaka mitano toka mwaka 2010 hadi mwaka huu zimekuwa zinapungua toka asilimia 54 mwaka 2010 hadi asilimia 24.1 mwaka huu jambo ambalo linaathiri unedeshaji wa shule.
“Fedha za uendeshaji wa shule kutokuja kwa wakati na mtiririko wa fedha hizi umekuwa ukipungua kwa kila awamu suala ambali linaathiri uendeshaji wa shule”alisema Bulenga.
Amebaisha kuwa katika kukabili changamoto hiyo wilaya inaendelea kuhamasisha jamii kuchangia fedha ili kufidia mwanya huu hata hivyo alikiri kuwa kasi ya uchangiaji ni mdogo.
Alisema kuwa wilaya inawasiliana na wizara ya Twala na za mikoa na serikali za mitaa na Hazina ili mgao wa fedha za uendeshaji wa shule utolewao uendane sawa na idadi ya wananfunzi waliopo shuleni na itumwe kwa wakati.
Akihutubia kwenye maadhimisho hayo mkuu wa wilaya ya Nachingwea,Paloleth Mgema aliwataka wadau wote wakiwemo viongozi wa kisiasa,watendaji wa halmashauri,walimu wazazi na jamii kwa ujumla kushirikiana katika kuzielewa na kuzifanyia kazi changamoto zilizobainika kukwaza kwa namna moja ama nyingine.
“Kutokuzielewa vizuri na kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo kunaweza kusababisha kuchelewa kuyafikia matokeo makubwa sasa (BRN) katika elimu”alisema Mgema.>>>SOMA ZAIDI HAPA

Post a Comment