WAZIRI wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, ametoa tamko kuhusu
mustakabali wa nchi kuelekea zoezi la kura ya maoni ya Katiba
Inayopendekezwa na uchaguzi mkuu ujao na namna matukio mengi yanavyoweza
kuibuka na kuashiria uvunjifu wa amani nchini.
Akizungumza
na wanahabari wizarani kwake leo, Chikawe alisema kuwa kila inapofika
wakati wa kuelekea chaguzi mbalimbali, kumekuwa kukitokea matukio
yanayoashiria uvunjifu wa amani yanayofanywa na watu ama vikundi vya
watu.
Alisema
matukio hayo yamekuwa yakisababishwa na hamasa za kisiasa au baadhi ya
watu ambao wamekuwa wakitumia muda huu kutekeleza ajenda zao za kihalifu
kwa kisingizio cha vuguvugu za kisiasa au yote mawili.
Alivitaka
vyama vya kisiasa kuepuka kufanya ushabiki wa kubeba wanachama wao
kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine wakati wanapoandaa mikutano
yao na badala yake wawashirikishe wanachama waliopo katika sehemu
wanapotaka kufanyia mikutano hiyo.
Chikawe
amesema hivi karibuni kumekuwa na matukio yanayotokana na baadhi ya
viongozi wa taasisi za dini kutoa matamko ambayo yanaashiria kuingilia
masuala ya kisiasa kinyume cha sheria ya vyama , sura ya 337 na kanuni
zake pamoja na katiba zinazosimamia uendeshaji wa taasisi hizo.
Alitoa
mifano ya viongozi wa taasisi za dini wanapokutana na kutoa matamko
yanayolenga kuwashawishi waumini wao wafuate maelekezo yao kuhusiana na
masuala ya Katiba Inayopendekezwa au kuhusu uchaguzi mkuu ujao, matamshi
ambayo yanakiuka sheria ya usajili wa taasisi hizo.
‘’Ni
kweli kuwa viongozi hao wa dini wana haki ya kushiriki katika masuala ya
kisiasa kama watu binafsi ila ni kinyume cha sheria kutumia uongozi
wao kuwashawishi waumini wao watekeleze matakwa yao ya kisiasa,’’
alisema Chikawe.
Alisisitiza
kuwa serikali itachukua hatua kali kwa watu binafsi, vyama vya siasa na
taasisi za kidini zitakazobainika kuvuruga usalama na utulivu wa nchi,
ikiwa ni pamoja na kufuta usajili wa vyama vya kijamii na vya kidini
ambavyo vitakiuka katiba ya kuanzishwa kwao.>>>>>SOMA ZAIDI
Post a Comment