Aliyekuwa
Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa Tiketi ya Chadema, Kabwe Zitto akisoma
barua aliyomwandikia Spika wa Bunge, Anne Makinda kumtaarifu kuwa
anang'atuka nafasi ya Ubunge. Pia aliwaaga Wabunge wenzake na kuahidi
kurudi tena Mungu akijalia baada ya Uchaguzi wa mwaka huu.
Mbunge
wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Zuberi Kabwe usiku huu ametangaza rasmi
Bungeni Dodoma kuachia kiti hicho alichokipata kupitia CHADEMA.
Mhe.
Kabwe ametangaza kung'atuka nafasi hiyo baada ya Mwenyekiti wa Bunge
Mhe Mussa Hassan Zungu Kumruhusu kutoa kauli binafsi mara baada ya
wabunge kumaliza kupitia vifungu vya sheria
ya Maafa ambayo hata hivyo haikupitishwa kwa kutotimia akidi ya wabunge ambao nusu yao hawakuwepo ukumbini.
ya Maafa ambayo hata hivyo haikupitishwa kwa kutotimia akidi ya wabunge ambao nusu yao hawakuwepo ukumbini.
Mhe
Zungu alimtakia kila la heri Mbunge huyo machachari ambaye amesema
ameamua kuachia ngazi baada ya chama chake kumfukuza. Hata hivyo
alimalizia kwa kusema kwamba anategemea kuwa nao tena mwezi Novemba
mwaka huu.CHANZO : MTAA KWA MTAA BLOG
Post a Comment