Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amemtaja
mfanya biashara huyo kuwa ni Obed Masawe, (50) ambae anamiliki duka la
kuuza vinywaji vikali ,maarufu Masobe Treders, lililopo jengo la Chama
cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Arusha.
Amesema mfanyabiashara huyo ambae ni mkazi wa Njiro jijini
Arusha,alifikwa na mauti akiwa kwenye klabu ya wafanyakazi wa Benki kuu
ya Tanzania, BOT,alipokuwa akiendelea kunywa bia.
Sabasi alisema tukio hilo limetokea Machi 23 mwaka huu, majira ya saa
1.30 usiku,ghafla alijisikia vibaya, na taarifa za awali zinaonyesha
kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa presha.
Katika tukio lingine Kamanda, Sabas, alisema mwanamke mmoja
anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 25, alikutwa amefariki dunia
na mwili wake kusokomezwa kwenye mtaro wa maji ya mvua jana, katika
makutano ya bara bara ya Makongoro na Azimio, jirani na jengo
la CCM Mkoa.
Alisema mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa hospital ya mkoa ya Mount Meru, ukisubiri ndugu kujitokeza kumtambua.
Aliongeza kuwa marehemu huyo ambae hajafahamika, mwili wake uligundulika baada ya kutoa harufu .
Uchunguzi unaendelea kufahamu vyanzo vya vifo hivyo.
Post a Comment