0
TAARIFA KUHUSU KUANZA KWA MKUTANO WA
19 WA BUNGE JUMANNE IJAYO
Mkutano wa Kumi na Tisa wa Bunge la Kumi
ambao ni mahusisi
kwa ajili ya Kushughulikia Miswada ya Sheria,
unatarajiwa kuanza siku ya Jumanne
tarehe 17 Machi 2015 na kumalizika tarehe 1
April 2015 Mjini Dodoma. Shughuli
zitakazokuwepo katika Mkutano huo ni kama
ifuatavyo:
1.0 MISWADA
YA SHERIA:
1.1
MISWADA
YA SHERIA YA SERIKALI:
a) Kusomwa
kwa mara ya Kwanza na hatua zake zote:
Katika Mkutano huo, Kwa mujibu wa Kanuni
ya 93(3) ya Kanuni za Bunge Toleo la Aprili
2013 Jumla ya Miswada Sita (6) itawasilishwa
Bungeni kwa Hati ya Dharura na inakusudiwa
kupitishwa na Bunge katika hatua zake zote.
Miswada hiyo
ni:
(i)
Muswada wa Sheria ya kupata habari wa
Mwaka 2015(The Access to Information Bill,
2015),
(ii)
Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari wa
Mwaka 2015 (The Media Services Bill, 2015),
(iii)
Muswada
wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya
Ushindani wa Mwaka 2015 [The Fair Competitio
(Amendment) Bill,
2015],
(iv)
Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao wa
Mwaka, 2015(The Computer and Cyber Crimes
Bill, 2015),
(v)
Muswada
wa Sheria ya Miamala ya Kiektoniki wa Mwaka
2014 (The Electronic Transaction Bill, 2015),
(vi)
Muswada
wa Sheria ya Gesi Asilia wa Mwaka 2015 (The
Natural Gas Bill, 2015).
b) Kusomwa
kwa mara ya Pili na hatua zake zote:
Aidha, Jumla
ya Miswada 15 itasomwa kwa mara ya Pili
Bungeni na kupitishwa na Bunge katika hatua
zake zote kwa mujibu wa Kanuni ya 86(1) ya
Kanuni za Bunge. Miswada hiyo ni:
(i)
Muswada
wa Sheria ya Udhibiti wa Ajira za Wageni wa
Mwaka 2014 [The Non- Citizens Employment
Regulation Bill, 2014];
(ii)
Muswada
wa Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa
wa Mwaka 2015 [The National
Payment Systems Bill, 2015],
(iii)
Muswada
wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa Mwaka
2014 (The Tax Administration Bill, 2014.
(iv)
Muswada
wa Sheria ya Takwimu wa Mwaka 2014 (The
Statistics Bill, 2014),
(v)
Muswada
wa Sheria ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI wa
Mwaka 2014 [The Tanzania Commision for
AIDS (Amendment) Bill, 2014],
(vi)
Muswada
wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa wa
Mwaka 2014 [The Disaster
Management Bill, 2014],
(vii)
Muswada
wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Dawa
za Kulevya wa Mwaka 2014 [The Drug Control
and Enforcement Bill,
2014],
(viii)
Muswada
wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya
Stakabadhi Ghalani wa Mwaka 2014 [The
Wharehouse Receipts (Amendment) Bill,
2014],
(ix)
Muswada
wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya
Uhamiaji wa Mwaka 2014 [The Immigration
(Amendment) Bill, 2014],
(x)
Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Silaha wa
Mwaka 2014 [The Firearms and Ammunition
Control Bill, 2014],
(xi)
Muswada wa Sheria ya Wataalam wa Kemia wa
Mwaka 2014 [The Chemist Professionals Bill,
2014],
(xii)
Muswada
wa Sheria ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali wa Mwaka 2014 [The Government
Chemistry Laboratory Bill,
2014],
(xiii)
Muswada
wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali
(Na. 2) wa Mwaka 2014 [The Written Laws
(Miscellaneous
Amendements) (No. 2) Bill, 2014] ,
(xiv) Muswada wa Sheria ya Bajeti wa Mwaka
2014 [The Budget Bill, 2014], na
(xv)
Muswada
wa Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania wa
Mwaka 2015 [The Youth Council of Tanzania
Bill, 2015],
1.2
MUSWADA
BINAFSI WA MBUNGE:
kwa Mujibu wa kanuni ya 81 (1) ya
Kanuni za Bunge, katika Mkutano ujao wa 19
kunatarajiwa kuwasilishwa
Muswada Mmoja wa Mbunge Binafisi ambao ni
Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana
la Taifa wa Mwaka 2013 (The Nationa Youth
Council Bill, 2013) wa Mheshimiwa John John
Mnyika. Muswada huu utasomwa
kwa mara pili na hatua zake zote.
2.0 MAAZIMIO
NA ITIFAKI MBALIMBALI
Pamoja
na Miswada hiyo, katika Mkutano wa 19, Bunge
linatarajia pia kuazimia Maazimio Mawili
kama ifuatavyo:
1.
Azimio la kuridhia Mkataba wa Msingi na
Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala
Barani Afrika.
2.
Azimio la kuridhia Makubaliano ya Msingi
ya Ushirikiano katika Bonde la mto Nile
(Agreement
on the Nile river basin Co-operative
Framework- CFA).
3.0 MASWALI:
Aidha, katika
Mkutano huu wa 19 wa Bunge, Jumla ya
Maswali ya kawaida 170 yanatarajiwa kuulizwa
na kujibiwa ambapo ni wastani wa
Maswali 15 kwa siku na maswali 10 kwa siku
za Alhamisi.
Aidha kutakuwa
na kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu kwa
Mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ambapo jumla
ya Maswali 18 ya msingi yataulizwa na
kujibiwa na Mhe. Waziri Mkuu.
Ratiba Kamaili
ya Mkutano wa Kumi na Tisa (19) na jinsi
shughuli zitakavyowasilishwa itatolewa
baada ya Kamati ya Uongozi kukutana
Jumatatu tarehe 16 Machi, 2015 ambapo
itatolewa na kuwekwa katika Tovuti ya Bunge
ambayo ni www.parliament.go.tz
Imetolewa na:
Idara ya
Habari,Elimu kwa Umma na Uhusiano wa
Kimataifa,
Ofisi Ndogo za
Bunge
DAR ES SALAAM

Post a Comment

 
Top