0

BEKI ALIPOOSHA KICHWA CHA MSHAMBULIAJI BADALA YA MPIRA

Mchezaji wa timu ya Herediano alikimbizwa hospitali baada ya kupigwa buti kichwani wakati wa michuano ya ya Ligi ya Mabingwa Amerika Kusini chini ya Shirikisho la Soka barani humo (Concacaf).Mechi hiyo ya nusu fainali kati ya Herediano ya Costa Rica dhidi ya Club America tukio hilo liliwashitua wengi uwanjani hapo.Huku dakika zikiwa zinayoyoma, beki wa Club America Paolo Goltz alikuwa akiosha mpira lakini buti lake liliishia kichwani mwa Cristhiam Lagos.


Post a Comment

 
Top