Mwaandishi wetu
Baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi limeanzimia kuchukua eneo la ardhi hekari 800 zinazodaiwa kumilikiwa ya Shirika la mafuta na petro TPDC kwa miaka 30 kinyume na sheria.
Akizungumza kwenye kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Maimuna Mtanda alisema kuwa shirika la mafuta la Taifa (TPDC) limekuwa likimiliki eneo kwa madai ya kupewa kampuni ya Kilamko kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha Sement
Alisema kuwa halmashauri imefanya jitihda ya kufutilia usajili wa kampuni ya Kilamco ambayo ilikuwa ina miliki eneo hilo kwa msajili wa makampuni breella, lakini alipofika huko uongozi ulimueleza kuwa hakuna kampuni iliyosajiliwa kwa jina hilo.
“kwa kweli ofisi yangu kupitia idara ya ardhi tunaendelea kufutitilia ili kupata ukweli wa mmiliki wa halali kati ya shirika la Mafuta na Petroli na Kilamko”alisema Mtanda .
Mtanda alisema shirika la Taifa la mafuta. petroli walikuwa wanaushirkiano wa kikazi, na kampuni hiyo na kuchukuwa ardhi hiyo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda miaka 30 iliyopita.
Naye Diwani wa kata ya Mitole Rafii Kuchao alisema kuwa kodi ya halmashauri inapotea ya shs bil.3 mpaka sasa tangu eneo hilo limechukuliwa bila kundelezwa
Kuchau alisema kuwa TPDC ni tatizo kwa hiyo vyombo vya ulinzi na usalama vitumike kuweza kupatikana kwa kodi hiyo ya shs.bil 3 za kodi ya ardhi ili ziweze kusaidia, miradi mbalimbali ya maendeleo , wilayani humo.
Aidha Mwaka 2014 kulifanyika vikao vya baraza la madiwani halmashauri na uongozi wa shirika la Taifa la mafuta na Petroli (TPDC) walikubaliana kwa pamoja kugawana ardhi ya hekali 800 kwa kila mamlaka ipatiwe hekali 400.
Hata hivyo halmashauri hiyo ilikataa pendekezo hilo na kuwataka TPDC kuandaa kikao cha makubaliano ili waweze kujadili suala hilo na kulitafutia ufumbuzi
Post a Comment