:Wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Al Shabaab wameshambulia mkahawa mmoja mjini Mogadishu na kua watu 10
Kundi
la wapiganaji linaloshukiwa kuwa sehemu ya wanamgambo wa Al Shaabab ,
limevamia hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Wanajeshi wa serikali ya Somali wanaendelea kupambana na wanamgambo hao waliojihami kwa vilipuzi na bunduki za rashasha.
Watu 10 wameripotiwa kuuawa katika uvamizi huu.
Kwa
mujibu ya walioshuhudia wapiganaji hao wa Al Shabaab walishambulia
hoteli ya Maka al-Mukarama mjini Mogadishu moja katia ya hoteli maarufu
mjini humo ambayo inapendwa na wengi wa wafanyikazi wa kimataifa na
mabalozi.
Aidha balozi wa Somalia nchini uswisi Yusuf Bari Bari alinusurika kifo baada ya kukwepa kupitia dirishani.
Kikosi
maalum cha kupambana na uvamizi wa aina hiyo kinaendelea kukabiliana na
wapiganaji hao ambao wanasemekana kuwa wamebanwa katika orofa ya juu
ambapo sasa wanarusha grenedi na kufyatua risasi kwa yeyote anayeonekana
kuwavizia.
Afisa
wa Polisi anayeongoza operesheni hiyo meja Ismail Olow ameiambia
shirika la habari la Reuters kuwa kati ya wavamizi 9 waliotekeleza
mashambulizi haya 6 tayari wameshauawa.
Kundi
la Al Shaabab limekuwa likitekeleza mashambulizi ya aina hii katika
hoteli zinazosifika kuwa mahala pa burudani kwa wageni na viongozi
mashuhuri serikalini.
Shambulizi hili la leo linafuatia lingine lililoanza kwa bomu yapata mwezi mmoja uliopita nje ya hoteli hiyo.Bbc swahili
Post a Comment