Meya wa manispaa ya ilala Mhe.Jerry Silaa akiwasikiliza wananchi na
watendaji waliofika kushuhudia yeye na timu nzima ya watendaji wa
manispaa ya ilala wakiwa katitka daraja la ukonga mazizini baada ya
kufanya ziara ya ghafla katika eneo hilo kushuhudia maendeleo ya ujenzi
wa daraja hilo alilowaahidi kujengwa kabla ya kipindi cha uchaguzi mkuu
ujao...
Msikie meya Huyu wa ilala hapa tunamnukuu....
''Tumehamishia ofisi Mombasa Mazizini....
Meya,Naibu Meya, Mkurugenzi,Mwekahazina,Mhandisi,Mwanasheria,Mepo,Diwani,Wenyeviti wa Mitaa....
Naamini suluhu itapatikana. Daraja hili limejengwa kwa taarifa ya
mwananchi tu....Hiyo ni kauli ya mstaiki meya wa Ilala mhe.Jerry Silaa
wakati alipohamishia ofisi nzima(watendaji)wa manispaa yake katika eneo
la Ukonga mazizini linapojengwa Daraja ambalo limeshakuwa kero kwa
wananchi wa ukonga zaidi ya miaka kumi..Hongera sana Jerry Silaa kwa
kazi nzuri na ya mfano kwa wanchi wa Ukonga na manispaa ya Ilala kwa
ujumla.
Post a Comment