Na Frank saidi Lindi :
WANANCHI wa kijiji cha Kitohavi,kata ya Matimba, wilaya ya ya Lindi
vijijini,wamemzuia mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya hiyo,Nyamande
Kazimil,kumuapisha Rashidi Abdallah Naveti (CCM) kuwa mwenyekiti wao,kwa madai
hawakumchagua katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopita.
Habari kutoka
kijijini humo na kuthibitishwa na baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi huo,na
uongozi wa Halmashauri hiyo,zinaeleza tukio hilo, limefanyika Ofisi ya kata
hiyo,mwishoni mwa wiki iliyopita.
Wakizungumza na
mwandishi wa gazeti hili kijijini hapo,baadhi ya wakazi hao,Isumaili Juma,Ashura
Selemani na Kindamba Kaisi kwa nyakati tafauti walisema katika uchaguzi wa
serikali za mitaa uliopita waliomchagua mgombea wa Chama cha
wananchi (CUF) Rashidi Kionjo kuwa kiongozi wao.
“Katika uchaguzi huo
sisis tumemchagua Kionjo wa (CUF) kuwa mwenyekiti wetu,lakini siku ya kuapishwa
limepelekwa jina la Rashidi Naveti wa (CCM) hapo ndipo tusipokubali kuletea
kiongozi tusiemchagua”Walisema wakazi hao.
Aidha,walisema siku
ile ya upigaji kura uliofanyika mwishoni mwa mwaka uliopita,msimamizi msaidizi
wa uchaguzi huo,Abdallah Ngoleka alimtangaza Rashidi Kionjo wa (CUF) kuwa ni
mshindi katika uchaguzi huo kwa kupata kura (60) na kumshinda mpinzani
wake,Rashidi Naveti wa (CCM) aliyepata kura (44).
Pia,wakaeleza katika
uchaguzi huo,wagombea wote wawili wa (CUF) na (CCM) Waliweka saini zao katika
Fomu ya matokeo wakiyakubali matokeo ya uchaguzi huo,huku nyingine
zikibandikwa kwenye mbao za matangazo zilizopo katika Ofisi hiyo ya serikali ya
kijiji.
“Wagombea wote
waliweka saini zao kuyakubali matokeo hayo, chakushangaza siku ya uapishaji
limepelekwa jina la Rashi Naveti wa (CCM) ambae hakushinda katika uchaguzi
ule”Alisema Kionjo ndiye ali
Aidha,walisema
kutokana na mtafaruku huo,mwanasheria huyo aliwaapisha wenyeviti wa vijiji vya
Likwaya, Moka, Matimba, Kikomolela,Komoro na Makumba,wakiwemo na wenyeviti wa
vitongoji na wajumbe.
Wakizungumza kwa
nyakati tafauti na gazeti hili,mgombea Rashi Kionjo wa (CUF) alisema
anachotambua yeye ndiye mwenyekiti mpya wa serikali ya kijiji hicho,baada ya
kupata ushindi wa kura (60) zidi ya (44) za mgombea wake wa (CCM) Rashidi
Navet.
Hata
hivyo,mwanasheria huyo alipofuatwa na mwandishi wa gazeti hili,ili kupata kauli
yake hakuwa tayari kutoa ushirikiano na kumtaka aende kuonana na uongozi wa
halmashauri ya wilaya hiyo.
Mwandishi wa Gazeti
hili alipofika Ofisi ya Halmashauri hiyo,ili kupata kauli ya mkurugenzi
mtendaji wake,Oliver Umberto Vavunge,alijibiwa na sektari wake kuwa yupo kwenye
kikao,hivyo ni vigumu kuweza kumpata kutokana na kutingwa na majukumu ya
kikazi.
Zoezi la uhapishaji
lilikuwa lifafanywe wiki iliyopita kwenye ukumbi wa Ofisi ya kata ya Matimba,na
mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya hiyo ya Lindi vijijini,Nyamande Kazimil.
Gazeti hili
limefanikiwa kupata baadhi ya Fomu za matokeo ya uchaguzi huo,ambazo
zinaonyesha watu 126 walijiandikisha kupiga kura,ambapo 124 walijitokeza
kutekeleza zoezi hilo,huku mgombea wa (CUF) akipata kura (60) na wa (CCM)
ikiambulia (44) tisa zikiharibika,hata hivyo takwimu hizo zinaonyesha utata
kwani kura (11) hazijuikani ziliko
Post a Comment