0


Morogoro. Shahidi watatu katika kesi inayomkabili Kiongozi wa jumuiya na taasisi za kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda ametoa ushahidi wake katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro huku mawakili wa upande wa mashtaka na upande wa utetezi wakisigana kwenye kifungu cha 150 hadi 152 cha sheria ya ushahidi.


Pande hizo mbili zilivutana katika kifungu hicho baada ya Wakili wa Upande wa utetezi Abubakar Salim kuiomba mahakama kutoa maamuzi kwa kile alichodai kuwa Wakili wa upande wa mashataka unamuuliza shahidi maswali ya muongozo kupitia maelezo ambayo yalitolewa na shahidi aliyepita bila ya kuiomba ruksa mahakama.


Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Mary Moyo, shahidi huyo ambaye ni askari polisi mwenye namba F4103 PC Ernest anayefanyakazi kwenye chumba cha mashtaka katika kituo kikubwa cha Polisi mkoa wa Morogoro aliieleza mahakama kuwa Agosti 10 alipokea maelezo kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Morogoro Rco Jafert Kibona yanayohusu kesi ya uchochozi inayomkabili Sheikh Ponda.


Akiongozwa na wakili wa Serikali George Mbalasa shahidi huyo alieleza kuwa baadaye alifungua kesi yenye namba RB/8684/2013 na IR/4473/2014 kisha alichukua maelezo mafupi yaliyoandikwa na Rco ambaye alikuwa kama mlalamikaji kisha kuyaweka kwenye jarada la kesi hiyo.


Wakili Juma Nassoro wa upande wa utetezi alimuuliza maswali shahidi huyo ili kutaka kujua kama alikuwepo eneo la tukio hata hivyo shahidi huyo alidai hakuwepo eneo la tukio bali alifungua kesi baada ya kupata maelezo kutoka kwa mkubwa wake wa kazi ambaye ni Rco.


“Mbali na Rco je nani mweingine alikuja kufungua kesi ama kulalamika kuhusu kesi inayomkabili Sheikh Ponda, na je ushahidi anaoutoa unauhusiano gani na ushahidi uliotolewa na mashahidi wengine waliopita katika kesi hiyo” aliuliza Wakili Nassoro. CHANZO:MWANANCHI

Post a Comment

 
Top