MAABARA, PICHA KUTOKA MAKTABA
Na mwaandishi wetu
Nanyumbu,Halmashauri ya wilaya ya
Nanyumbu mkoani Mtwara imepongezwa kwa ushirikiano unaofanywa baina ya
watendaji na mkurugenziHalmashauri hiyo na wadau mbalimbali katika kutekeleza
agizo la Raisi Jakaya Kikwete la ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule za
sekondari za kata ambapo zipo katika hatua za kuridhisha.
Akizungumza wakati wa majumuisho yaliyojuisha wadau
mbalimbali mwamnzoni mwa wiki mkuu wa mkoa wa Mtwara,Halima
Dendego
alisema amejionea na kuridhishwa na
utekelezaji unaofanywa wa watendaji wa halmashauri kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali na luwaomba waendelee na jitihada hizo hadi kuhakikisha
wanakamilisha ujenzi huo.
“Nawapongeza sana kwa kazi bora ya
ujenzi wa maabala naamini ubora huu niliouona kwenye maabala hizi ni
ushirikiano wa pamoja kwenu viongozi wa wilaya lakini pia wananchi nao
wamethubutu kujitoa kuleta maendeleo kwenye kata zao hongereni sana,” alisema
Dendegu
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu,Ally Kasinge alisema kuwa Halmashauri yake
ina shule 12 za sekondari za kata na maabara 36 ambapo kabla ya agizo la
serikali la ujenzi wa maabara ilikuwa na maabala 7 ilianza kwa kujenga maabala
nane na sasa imeshajenga maabala 21 ambapo hadi Machi 30 mwaka huu zitakuwa
zimeshakamilika.
Kasinge alisema kuwa maabala nane
ambazo zimejengwa zinagharama ipatayo Sh.314,680,000 ambapo wamechangia Sh.50.4
milioni kama nguvu kazi kutoka kwao na Halmashauri imechangia Sh.181.9 milioni
huku mchango kutoka serikali kuu ni 82.38
Alisema kuwa hadi kukamilisha ujenzi wa
maabala zote 21 zinazoendelea kujengwa ni kwamba jumla ya Sh.1.5 bilioni
zitahitajika ili kufanikisha ujenzi huo na kwamba kila maabala moja inagharimu
Sh.72.4
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.