Mwanza. Usafiri wa meli kati ya Mwanza na Kagera, upo shakani kutokana na kutokamilika mapema matengenezo ya Meli ya MV Serengeti, inayochukua nafasi ya MV Victoria iliyosimamisha safari kutokana na ubovu.
Awali, Kampuni ya Huduma za Meli Mwanza (MSCL),
ilisema matengenezo hayo yangekamilika katikati ya mwezi huu, lakini
imeshindikana kutokana na ukosefu wa fedha.
Meli ya MV Serengeti ina uwezo wa kubeba abiria
593 na tani 350 za mizigo, ilitarajiwa kuanza safari katikati ya mwezi
huu baada ya kusimama kwa Meli ya MV Victoria.
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(Sumatra), ilitoa amri ya kusitisha safari za Victoria Desemba 19 mwaka
jana baada ya kupata hitilafu kwenye injini zake mbili.
Kutokana na tatizo hilo, uongozi wa MSCL uliamua
Meli ya MV Serengeti, iliyokuwa ikisafirisha mizigo kwenda Uganda
ibadilishwe na kubeba abiria, huku ikitakiwa kwanza kufanyiwa
marekebisho.
Akizungumza ofisini kwake juzi, Meneja wa MSCL
Tawi Mwanza, Phillemon Bagambilana alisema meli hiyo inafanyiwa
matengenezo makubwa na madogo, jambo ambalo limeifanya kutumia muda
mrefu.
“Matengenezo makubwa ni yale yanayohusisha
kubomolewa injini zote mbili na kuziunda upya na jenereta mbili
zinazotumika kwa ajili ya kusambaza umeme.
“Matengenezo madogo ni kuiweka katika sura ya kubeba abiria kwa maana ya kupaka rangi, kuwaandalia abiria mazingira mazuri ya kukaa na kuweka huduma zote muhimu,” alisema Bagambilana.
“Matengenezo madogo ni kuiweka katika sura ya kubeba abiria kwa maana ya kupaka rangi, kuwaandalia abiria mazingira mazuri ya kukaa na kuweka huduma zote muhimu,” alisema Bagambilana.
Alisema licha ya jitihada wanazofanya kuhakikisha
wanamaliza kazi kama walivyopanga, matengenezo hayo yanatarajiwa
kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.
Bagambilana alisema matengenezo yake yanakwenda
taratibu kwa sababu ya kutopata vifaa kwa wakati, huku wakikosa fedha za
kutosha za kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi.
“Kwa sasa injini moja imekamilika, tunatengeneza
ya pili na jenereta mbili za umeme matengenezo yake yanaendelea ila
hayajakamilika,” alisema Bagambilana.
Mmoja wa wakazi wa Kagera, mfanyabiasha wa ndizi, Lutha Victor, alisema tangu kusitishwa kwa huduma za meli, hali imekuwa mbaya.MWANANCHI
Post a Comment