
Na Mwaandishi Mtwara
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendegu, ameonesha kutoridhishwa na
ufugaji wa unaofanywa katika shamba la kuzalisha mitamba ya ng’ombe
lililopo katika ya wilaya ya Nanyumbu mkoa wa humo na kuahidi kuwatuma
wataalamu wa mifugo toka ofisi yake ili wahainishe fursa zilizopo na namna ya
kuboresha ili kukiwezesha kujiendesha bila ya kutegemea ruzuku ya serikali.
Akizungumza na
watumishi wa shamba hilo jana(jumamosi) wakati wa ziara yake ya kikazi
aliyofanya wilayani humo mkuu wa mkoa huyo alionyeshwa kushangazwa namna
mifugo wanavyofugwa kwa kutumia njia zisizo na ubora hali ambayo
ufugaji wa namna hiyo hautawaletea tija.
Alibainisha kuwa
haoni sababu ya kituo hicho kuendelea kujiendesha kwa kutegemea ya ruzuku
ya serikali wakati kinauwezo wa kutumia fursa zilizopo kwa kuzalisha mitamba
kwa wingi na kuiuza kwa wananchi ambao bado wanahitaji mitamba hiyo.
Alisema kuwa shamba
hilo linafursa nyingi ikiwemo eneo zuri lenye nyasi na maji ya kutosha na kuwa
iwapo zitatumika vizuri zitawezesha kuboresha ufugaji na kuwa wenye tija
na kuzisadia wilaya zinazotegemea shamba hilo kupata ngombe wa kufuga .
“Kwa kweli kwa
haraka nimeona zipo fursa nyingi hapa lakini tatizo hamzitumii
vizuri hivyo nitawaleta wataalamu kutoka ofisi yangu ili waziahinishe na
kuona namna zitavyosaidia kuleta tija”alisema Dendego.
Alisema kwa
kutumia fursa hizo zitakazoainishwa na wataalamu wa ofisi yake
atazishirikisha halmashauri zote mkoani kuona namna ya
kuchangia katika kuboresha shamba hilo ambalo ndilo
tegemeo kubwa kwa wananchi wa mikoa ya Lindi,Mtwara na wilaya ya Tunduru
mkoa wa Ruvuma.
Kwa upande Meneja wa
shamba hilo Issa Hamisi Nambwalaja alisema kuwa ufinyu wa bajeti
umesababisha shughuli nyingi za maendeleo kukwama ikiwemo ununuzi wa
ng’ombe wazazi,ununuzi wa trekta mpya na vifaa vya kuvunia na
kufyekea wa vichaka na kuiomba serikali kupeleka kwa wakati.
Post a Comment