Baada
ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kutangaza kusogeza mbele zoezi la
uandikishwaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wamezungumzia juu uya suala hilo.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Libuva
alitangaza hatua hiyo wakati wa mkutano wa pamoja baina ya viongozi wa
vyama vya siasa na NEC kujadili zoezi la uandikishwaji wapiga kura
katika daftari la kudumu la wapiga kura chini ya mfumo mpya wa
electronic (BVR).
“Kwa
kweli tuna matatizo makubwa kwa sababu pamoja na kukutana na tume ya
uchaguzi ya taifa na kuelezwa kwamba sasa uchaguzi wa kujiandikisha
utaanza tar 23 katika mkoa wa Njombe hatukupata fursa wala hatukupewa
ratiba kamili ya uandikishwaji wa wapiga kura katika maeneo yote vile
vile hatukupewa ratiba kamili ya vituo vya kuandikishia wapiga kura hapa
Njombe na mikoa mingine” Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba
“Ni
kweli NEC imesogeza mbele uchaguzi haujafanyika… mimi naona ni sahihi
kwa sababu najua huu mfumo haujaeleweka … nashukuru kama tumekukubali
kuongeza wiki moja ili tuendelee kujielimisha kuhusu mfumo na kuona
namna gani tutashiriki kikamilifu bila kuja kupata matatizo mbele ya
safari“– Augustine Mrema, Mwenyekiti wa TLP.
“Uboreshaji
wa daftari la kudumu la wapiga kura ni hatua ya msingi sana katika
kuhakikisha uchaguzi mkuu ujao lakini hata kura ya maoni ya katiba
inayopendekezwa inakuwa huru inakuwa haki na inashirikisha watu wengi..
mchakato wa kuliboresha daftari hili usipoenda vizuri unaweza
ukasababisha nchi yetu ikachafuka na tunayo mifano mingi katika nchi
nyingine. Uamuzi wa kusongeza mbele kwa lengo la kuboresha mchakato
mzima ni umauzi wa busara… tujihakikishie kwamba zoezi litakwenda vizuri
kila anayetakiwa kushiriki ataridhika” Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM.
Post a Comment