Viongozi wa halmashauri ya wilaya Nachingwea wakiwa kwenye kikao za baraza la madiwani
KUWA DC WA JK
ATANGAZA KUTOGOMBEA
Mwaandishi wetu,Nachingwea.
Februari 03:MWENYEKITI wa Chama cha mapinduzi {CCM} wilaya ya
Nachingwea,mkoani Lindi,Albert Mnali,amevunja ukimya na minong’ono iliyokuwa
ikiwasumbua wananchi kwa muda wakiwemo baadhi ya wanachama wa Chama hicho,kwa
kuweka bayana kwamba hayupo tayari kugombea ubunge wa Jimbo hilo.
Kiongozi huyo wa kisiasa ametoa kauli hiyo,alipokuwa
akizungumza katika mahojiano maalumu na timu ya waandishi wa Habari wa vyombo
mbalimbali vilivyomtembelea nyumbani kwake mjini Nachingwea.
Mnali ambaye aliwahi kuwa mkuu wa wilaya mbalimbali hapa nchini,ikiwemo ya kagera,kasha kufutwa
kazi na Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa madai ya kuwacharaza viboko
walimu,amekanusha madai ya yeye kutaka kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo
hilo la Nachingwea katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwaka huu.
Amesema kimsingi yeye hafikirii na hana mpango wa kutaka kugombea
nafasi hiyo ya ubunge,kwani macho na mawazo yake ni kutaka kukioongoza Chama
hicho hadi pale wanachama watakapoamua kumpumzisha kupitia uchaguzi wa ndani ya Chama hicho.
Mnali akasema kwa sasa ni muda wa kupisha damu change kuongoza
ili kuweza kukabiliana na changamoto za wakati huu,na yeye atabaki na kuendelea
kuwa mshauri.
“Nadhani ni vema basi kupisha damu change ili ziweze kukabiliana
na changamoto za wakati huu,kwani kwa mimi sasa natakiwa kuwa mshauri zaidi mshauri
badala ya kazi za utendaji”Alisema Mnali.
Kiongozi huyo wa kisiasa ni miongoni mwa wanachama wanaotajwa
kuwania kuomba ridhaa ya wananchi kutaka kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu
wa madiwani,wabunge na Rais unaotarajia kufanyika mwaka huu.
Wanachama makada wanaotajwa kuwania Jimbo hilo ambalo kwa
sasa linashikiliwa na waziri wa mambo ya ndani,Mathias Chikawe,ni pamoja na mkuu
wa wilaya ya Kilombero,Hassani masala,kamanda wa vijana (UVCCM) wilaya ya
Nachingwea,Stepheni Nyoni,Katibu wa (CCM) wilaya ya Mkuranga,mkoani Pwani,Issa
Mkalinga,mlezi wa Chipukizi wa wilaya hiyo,Gaston Owino Onyango.
Post a Comment