PICHA KUTOKA MAKTABA
Mwaandishi wetuLindi….
Mtoto Farisi Yusufu Alife (15)
mkazi wa Kiwanjani kata ya Nyengedi, Wilaya ya Lindi,amewashitaki kwenye baraza
la kata wazazi wake wawili kwa kutompeleka shule kwa ajili ya kuendelea
na masomo yake ya kidato cha kwanza.
Akizungumza na mwandishi na timu ya
waandishi wa habari waliotembelea kijiji hapo, mwanafunzi huyo Farisi
Yusufu,alisema amechukua maamuzi hayo baada ya wazazi wake kutoonyesha nia ya
kumpeleka shule ili kuendelea na masomo yake ya Sekondari.
‘’Ni kweli kwa mara ya kwanza
nimewafikisha wazazi wangu wawili yaani baba na mama Baraza la kata kufuatia
kutoonyesha niya ya kunipeleka shule,huku nikiwa nimefanikiwa kuchaguliwa
kuendelea na masomo ya Sekondari kata ya Mtua ‘’alisema Farisi.
Mwanafunzi huyo alisema baada ya kuwafikisha
katika Baraza hilo la kata na kutozwa faini y ash,10,000/- na kupewa amri
kuhakikisha wananipeleka shule mzazi wake hivi sasa yupo kwaenye maandalizi ya
kumpeleka ili akaendelee na masomo yake.
Baba mzazi wa mwanafunzi huyo,Yusufu
Alife amethibitisha kuwa yeye na mke wake Hadija Juma wamefikishwa katika
Baraza hilo la kata kwa kosa la kutompeleka kijana wake kuendelea na masomo
yake ya kidato cha kwanza.
’Nilikifikishwa mimi na mke wangu Hadija
Juma,lakini baada ya kusikiliza maelezo ya mwenzangu ,Baraza likaona mzigo hule
niubebe mimi na nikatozwa faini ya sh.10000/- na kama ningeshindwa
ilikuwa basi niende jela miezi mitatu’ alisema Alife.
Aidha,alitaja sababu zilizomfanya
asimpeleke kijana wake huyo shuleni ni pamoja na hali ngumu ya kiuchumi inayomkabili
ikizingatiwa ana motto mwingine anayemsomesha kidato cha tano shule ya
sekondari Mahiwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Baraza
hilo, Abdallah Malibiche,alikiri kuwa kijana huyo kuwafikisha wazazi wake hao
baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili ndipo Baraza likaamua kumtia
hatiani mzazi wa kiume na kumtoza faini hiyo au kifungo cha miezi mitatu
Jela.
‘’Mimi na wazee wenzangu wa Baraza baada
ya kusikiloiza maelezo ya pande zote mbili yaani mtoto na wazazi,likaamua
kumtia hatiani mzazi wa kiume kwasababu ndiye kichwa cha nyumba na pia
alikuwa akishauriwa na mke wake wampeleke shule kijana wao’’ alisema Malibiche.
Alisema shauri hiyo imepewa namba
02/BKN/2015, ambapo sababu zilizotolewa na wazazi hao kuwa na hali mgumu ya
kiuchumi,umepingwa na Baraza hilo na kuamuru alipe faini ya sh.10000/-
Kwa upande Afisa Mtendaji wa kata hiyo
,Thomasi Ngomo amempongeza mwanafunzi Farisi Yusufu kwa uwamuzi huo na kuwataka
watoto wengine kuiga mfano wake katika kutafuta haki zao za kupata elimu.
‘’Taarifa uliyoisikia ndugu mwandishi ni
ya ukweli kwani wote hao ni wazazi wa kata yangu hii ya Nyengedi kwa upande
wangu nampongeza huyu kijana kwa maamuzi aliyoyafanya kwa wazai wake na
ninawashauri watoto wengine kufuata nyayo hizo’’alisema

Post a Comment