Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya
Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza katika maadhimisho ya miaka
38 ya CCM, yaliyofanyika kitaifa juzi kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini
Songea, Mkoani Ruvuma.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya
Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula na Katibu Mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa maandalizi ya sherehe za
maika 38 ya Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mbunge wa
Songea mjini Dkt Emmanuel Nchimbi amesema kuwa chama chake kina kila
sababu ya kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa
kuwa kina mfumo na muundo imara.
Akizungumza muda mfupi baada ya
maadhimisho hayo mjini Songea, Dkt Nchimbi ambaye pia ni mjumbe wa
halmashauri kuu ya chama hicho alisema kuwa chama chake hakina tatizo la
kimfumo wa muundo na kuongeza kuwa ushindi ni lazima.
“Chama hakina tatizo la muundo wala mfumo
na tutakachofanya ni kubadilisha mikakati tu ili kujihakikishia ushindi
katika uchaguzi ujao,” alisema
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya
Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe katika maadhimisho ya miaka
38 ya CCM, yaliyofanyika kitaifa juzi kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini
Songea, Mkoani Ruvuma katikati ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo
Mwisho.
Aliongeza, “Kwa kwa kaida hakuna mkakati
unadumu. Mar a zote mikakati hubadilika kulingana na mazingira na hiki
ndicho tutakachokifanya,”
Akizungumzia kuhusu kauli ya mwenyekiti
wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete kuwataka viongozi wa chama
kuwatembelea wanachama na kushawishi wanachama wapya, alisema CCM ni
chama kikubwa na ndani yake wapo viongozi waliolala ambao mwenyekiti wa
taifa aliwakumbusha kuamka na kufanya kazi.
“Chama hakiwezi kuwa na maisha marefu
kama viongozi katika ngazi zote ha hawajitumi. Katika jeshi kubwa kama
hili la CCM wapo watu ambao lazima wasukumwe na ndiyo ahwa mwenyekiti
wetu wataifa aliwasukuma kupitia hotuba yake.
Hawa wanatakiwa kuamka na kuanza kufanya
kazi kwa bidii ili kukiwezesha chama kushinda kwa kishindo kama ambavyo
kimekuwa kikishinda tangu kuanza kwa siasa za vyama vingi,” alieleza
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya
Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana.
Dkt Nchimbi aliishukuru halmashauri kuu
ya chama kwa kuweza kuuchagua mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya maazimisho ya
miaka 38 ya chama hicho na kueleza kuwa kwa miaka mingi Ruvuma imekuwa
ngome imara ya CCM.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Ruvuma Oddo Mwisho alisema kuwa alisema kuwa chama chake kimeshaanza
kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu .
“Nimeshawaagiza viongozi wa chama katika
ngazi ya mkoa na wilaya kuanza vikao kwa ajili ya na kuweka mikakati
thabiti ya ushindi katika uchaguzi mkuu ujao,”
Alieeleza kuwa, chama katika mkoa wake
tayari kilishaanza mikakati ya kujitegemeza ikiwa ni kufuata agizo la
mwenyekiti wa taifa ambapo tayari kimejipanga vyema kuendeleza vyanzo
vyake vya mapato pamoja na kuanzisha vyanzo vipya kwa ajili ya kukifanya
kujitegemea.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya
Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) akijadiliana jambo na Makamu
Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa
chama hicho, Abdulrahman Kinana.

Post a Comment