Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.
Kwanza nianze makala haya kwa kumshukuru Mungu kwa kutupa uzima leo. Ahimidiwe daima.
Baada ya kusema hayo niseme wazi kwamba nchi yetu ilitikisika tena wiki iliyopita baada ya polisi wetu kuwapiga Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na wafuasi wake.
Baada ya kusema hayo niseme wazi kwamba nchi yetu ilitikisika tena wiki iliyopita baada ya polisi wetu kuwapiga Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na wafuasi wake.
Nchi yetu
inaongozwa kwa mujibu wa sheria na kanuni, haitakuwa busara kila mtu
kujifanyia mambo yake anayotaka bila kuzingatia sheria na hasa askari
wetu.Ningefurahi kama vyombo husika vitafanya uchunguzi wa kina kuhusu
suala hili na ikibainika kuwa polisi walitumia nguvu kubwa wawajibishwe
kwa mujibu wa sheria.
Binafsi
na wapenda amani wote katika nchi hii bila kujali itikadi za kisiasa
tunalaani vikali kitendo cha kupiga raia kama mbwa mwitu.
Naamini
yeyote aliyeona tukio lile kwa njia ya video alisikitika, alishangaa na
kuingia woga kwa sababu hakuna aliyekuwa anategemea kuona askari wetu
wakifanya vitendo ambavyo vilikuwa vikifanywa na askari wa Makaburu
dhidi ya Waafrika kule Afrika Kusini.
Kwa nini
askari umpige mtu ambaye ametii sheria au amri ya kukamatwa bila shuruti
wakati huo ndiyo msemo wa jeshi la polisi?Kwa tukio hili ni lazima
serikali isimamie sheria bila kupendelea mtu yeyote. Nasema hivyo kwa
sababu suala la amani ya nchi ni suala la kitaifa na halitakiwi
kuingizwa kwenye siasa, hivyo nawasihi viongozi wa polisi kuwa makini na
suala hilo ambalo limetia doa nchi yetu.
Nasema
limetia doa kwa sababu hata sasa ukifungua mitandao mbalimbali duniani
ikiwemo ya Voice of America (VoA), polisi wetu wanaonekana wakiwapiga
raia hata bila kujali wanapiga sehemu gani. Tumshukuru Mungu, hawakuua!
Lakini
yeyote aliyeona video ile ni lazima atapata hasira kwa askari wale
wachache waliokiuka sheria ya ukamataji raia waliokosa.Nisisitize tu
kwamba amani na usalama wa nchi yetu ni kitu muhimu sana katika ustawi
wa taifa letu, lakini kila siku tunashuhudia kuendelea kuporomoka kwa
amani na usalama, ninawasihi wananchi wenzangu, tunapojadili suala kama
hili lazima tuweke kando itikadi zetu, lengo likiwa kuliponya taifa.
Nisisitize
kuiomba serikali kufanya uchunguzi kupitia vyombo vyake, pia bunge
lichunguze sheria ambazo zinatoa mwanya wa vurugu ili kudhibiti vitendo
hivyo.Suala hili ni nyeti kwa sababu limeweka bayana kugongana kwa
mihimili mitatu ya nchi baada ya Bunge kujadili suala hilo wakati likiwa
limeshafika mahakamani.
IGP Mangu.
Mgongano huo umetokea katika kipindi kisichozidi miezi miwili baada ya
Bunge kugoma kupokea zuio la mahakama la kujadili kashfa ya uchotwaji
fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escow na kuendelea na mjadala ambao
ulifikia maazimio ya kuwawajibisha wahusika.
Sitamzungumzia Profesa Lipumba juu ya kukamatwa kwake Jumanne iliyopita
wakati akielekea Zakhem, Mbagala Dar kwa sababu shauri lake lipo
mahakamani.Licha ya shauri hilo kuwa mahakamani, wabunge walijadili kwa
kina tukio lote la kupigwa na kukamatwa kwa kiongozi huyo.
Ukweli ni kwamba Jeshi la Polisi Tanzania lilifanya haraka kuwahisha
shauri hilo mahakamani na kitendo hicho wachunguzi wa habari wanasema
kililenga kulizuia Bunge kutekeleza azma yake ya kujadili tukio hilo.
Jeshi la polisi halipaswi kutumia nguvu kuliko zinazohitajika katika
kukamata watuhumiwa wa makosa ya jinai hilo halipo kwenye sheria
naambiwa ipo kwenye maagizo ya jumla ya polisi yaani Police General
Orders.
Ukweli ambao upo wazi ni kwamba sheria haiwapi polisi mamlaka ya kupiga raia anayetii sheria au amri ya kukamatwa.
Ninachoweza kusema hapa ni kuwa kilichotokea kwa Profesa Lipumba
tusikichukulie kivyama bali tuangalie kwa upeo mpana wa kuendeleza amani
na ushirikiano kati ya polisi na raia na mali zao.
Namshauri Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu na safu
yake ya uongozi kwamba jeshi lake liepuke kuonekana kana kwamba bado
lina mfumo wa kikoloni ambao walikuwa wakikandamiza raia kwani linafanya
yale yale yaliyokuwa yakifanywa wakati wa ukoloni.
Nizidi kukushauri IGP Mangu kuwa sheria za polisi zibadilishwe kwa kuwa
zina mfumo wa ukandamizaji na kwamba ikibaki hivyo italiingiza taifa
kwenye maafa makubwa na ni hatari polisi kuwa adui wa raia wema.
Mwisho niwapongeze wabunge wote walioona athari ya kitendo kile hasa Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba ambaye alisema hata kama serikali inaundwa na CCM, lakini si kweli yanayofanywa na dola yote ni maagizo ya chama hicho.
Mwisho niwapongeze wabunge wote walioona athari ya kitendo kile hasa Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba ambaye alisema hata kama serikali inaundwa na CCM, lakini si kweli yanayofanywa na dola yote ni maagizo ya chama hicho.
Post a Comment