0


mechi imekamilika ikiwa Arsenal wameibuka kidedea kwa mabao 5-0 dhidi ya Aston Villa.

Arsenal imepanda hadi nafasi ya tano juu ya Tottenham katika ligi ya Uingereza baada ya kuicharaza Aston Villa mabao 5-0.
The Gunners walidhibiti mchezo na kuchukua uongozi baada ya Olivier Giroud Kupata pasi safi kutoka kwa Mesut Ozil.
Santi carzola alipiga chuma cha goli kabla ya mabao ya Mesut Ozil na Theo Walcot kufanya mambo kuwa 3-0.
Giroud alipiga chuma cha goli na kichwa kizuri kabla ya Carzola kufunga bao la Penalti baada ya mshambuliaji chuba Akpom kuangushwa katika eneo la hatari.
Hector Bellerin baadaye alifanya mambo kuwa 5-0 baada ya kusukuma mkwaju kimo cha nyoka.

Post a Comment

 
Top