Takriban
wavulana 40 na vijana wadogo wameripotiwa kutekwa nyara na wapiganaji
wa kundi la Boko haram Kazkazini mashariki mwa Nigeria.
Wakaazi
waliokitoroka kijiji cha Malari na kuwasili katika mji wa Maiduguri siku
ya ijumaa usiku wanasema kuwa kitendo hicho kilitekelezwa siku moja tu
kabla ya mwaka mpya.Wanasema kuwa watu waliojihami waliwasili katika kijiji hicho katika gari aina ya pick up na kuwaagiza wanaume wote kutoka nje ili kuweza kusikiliza mahubiri.
Vijana wadogo baadaye walizungukwa na kupelekwa katika msitu jirani wa Sambisa.
Mwaka uliopita kundi hilo la Boko haram liliwateka nyara zaidi ya wasichana 200 kutoka shule moja ya bweni kazkazini mwa Nigeria.BBC
Post a Comment