0

 

Na mwaansidhi wetu Kilwa

Wakulima wa wilaya ya Kilwa,  mkoani Lindi, wameiomba serikali  kuharakisha  mpango wa upimaji wa Ardhi kupitia mpango wa matumizi bora   katika maeneo yao  ili kuepuka migogoro ya wafugaji, wakulima na wawekezaji kwani inasabisha kurudisha nyuma juhudi za kupambana na umaskini kwa jamii.
Ombi hilo limetolewa kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Njianne,Somanga,Kiwawa, Mipingoni na Chang’ombe wilayani Ruangwa wakati walipokuwa wanazungumza na timu ya waandishi wa habari waliotembelea katika wilaya hizo.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji Miteja, wilayani humo Abrahamani Kachele anasema mpango wa pekee utakaokuwa suluhisho  lakupunguza migogoro ya ardhi ni  upimaji  wa matumizi bora ya ardhi.
Kachele anasema kutotengwa  kwa maeneo maalumu  ya wafugaji na wakulima  kumechangia  kuwepo kwa  kwa malumbano,migogoro na vurugu za kila mara zilizosababisha uharibifu wa mazao ya wakulima na mifugo. Anasema kuwa kwa mantiki hiyo hivyo ni vyema serikali ikaharakisha zoezi hilo la upimaji,
“Ni vema serikali ikatambua kuwa dawa pekee ya kuondoa migogoro ya ardhi  kati ya wafugaji na wakulima  ni mpango wa matumizi bora ya ardhi  na ili mpango huo uweze kukamilika  kwa wakati  ni vizuri kushirikisha wadau wate wanaoguswa  na hilo,” alisema Kachele.
Naye  Mkuu wa wilaya Kilwa,  Abdala Ulega, alisema wilaya yake imepima matumizi bora ya ardhi  kwa vijiji 14 ambavyo Njianne,Kiwawa,Somanga,Mitandi,Mavuji,Miteja,Mandawa, Singino  na Kilanjelanje kwa ajili ya shughuli za mifugo ambapo tayari wafugaji wanaishi katika maeneo hayo  bila ya kuingiliwa.

Post a Comment

 
Top