Klabu ya Yanga imepanga leo kuwasilisha malalamiko yao juu ya tukio la kunyanyaswa kwa mshambuliaji wake Amissi Tambwe kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lakini pia mchezaji husika amefafanua kwa kina juu ya manyanyaso anayoyapata.
Akizungumza mchana jana katika makao makuu wa klabu hiyo Mkuu wa Kitengo
cha Habari Jerry Muro amesema uongozi wao unakusudia kuwasilisha
malalamiko yao hayo ambayo mengi yametokana na vitendo alivyofanyiwa
Tambwe wikiendi iliyopita katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambapo
wanataka mapendekezo yao manne yafanyiwe kazi.
Muro amesema kwanza Yanga ingwetaka kuona TFF inawachukulia hatua kali
wahusika wote waliomdhalilisha Tambwe huku pili wakilitaka shirikisho
hilo kutoa hadharani taarifa ya tathimini ya waamuzi wa mchezo huo lengo
likiwa ni kujua umakini wa waamuzi hao.
“Tatu
tungewaomba wenzetu wa TFF kwa kuwa wao wapo kimya pia kuwachukulia
hatua wahusika wote waliosimamia mchezo huo kwa kushindwa kubaini haya
ambayo vyombo vya habari imeyafichua lakini ikiwezekana wafungiwe na
Yanga hatuwataki kuwaona wanachezesha mechi zetu vinginevyo tutagoma na
hata Ruvu nao tungependa kuona wanapewa adhabu kwa viongozi wao
kushabikia maovu haya.
Aidha
Tambwe mwenyewe amechukizwa na matukio hayo akisema ameshangazwa kuona
anafanyiwa vitendo vya kinyama ambapo mengine hawezi kuyaweka hadharani.
“Mpira ni
starehe mimi sikatai mchezaji anikabe lakini ni jinsi gani unanikaba
hapo ndiyo tatizo, naambiwa mimi mkimbizi hivi hawa wenzangu wanajua
maana na haya maneno yapo mengi ambayo nimedhalilishwa nayo kiungwana
siwezi kuyaweka wazi hapa lakini viongozi nitawaeleza,”alisema Tambwe
Post a Comment