WAZIRI wa
Ujenzi Dk. John Magufuli ameagiza kufungwa kwa mfumo mpya wa
kielektroniki katika vivuko vyote nchini ili kukabiana na wajanja
wachache wanahujumu mapato katika vivuko hivyo.
Mbali ya
hilo, ameagiza kufanywa kwa utaratibu utakaowezesha huduma katika vivuko
zinatolewa kwa saa 24 ili kukidhi mahitaji ya wananchi.
Dk.
Magufuli alitoa maagizo hayo jana katika uzinduzi wa mfumo mpya wa
kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na
Kampuni ya Africom Tanzania.
"Tulianze
pale Kigamboni na tukaona mafanikio, tulipokuja hapa (Kigongo)
tukaboresha na mafanikio yameonekana kwa kiasi kikubwa. Vivuko vyote
sasa vifungwe mfumo mpya wa kielektroniki...vivuko vyote nchini,"
aliagiza Magufuli.
Alisema
mfumo huo una faida kubwa ikiwemo kudhibiti upotevu wa mapato ambapo
katika kivuko cha kigongo – Busisi alisema mapato yameongezeka kwa
takribani asilimia 40 baada ya kufungwa kwa mfumo huo.
Hata
hivyo, Dk. Magufuli alikataa kutaja ni kwa shilingi ngapi mapato hayo
yameongezeka kwa hofu kuwa watu wenye dhmira mbaya wakisikia wanaweza
kwenda na kufanya uhalifu.
Pia, aliagiza Kivuko kwa Kigamboni nacho kiboreshwe mfumo wake kama ilivyokuwa kwa Kigongo – Busisi.
Waziri
huyo wa Ujenzi, alisema kutokana na mafanikio yanayopatikana katika
kudhibiti upotevu wa mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi,
wafanyakazi husika kwa maana ya wale wa TEMESA maslahi yao yanapaswa
kuangaliwa upya na kuboreshwa.
"Kama
mapato ni mazuri, wafanyakazi nao walipwe vizuri, wasikae kimasikini
kwani wanapaswa kuona mwaka 2015 ni ukombozi katika maisha yao.
Alisema
serikali chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete imefanikiwa kujenga
madaraja yote makubwa nchini ambapo kwa sasa kuna madaraja 4880 nchini
na kuwa wakati inapata uhuru kulikuwa na madaraja mawili ambayo yalikuwa
ya kuvutwa.
Mfumo wa
kielektroniki katika vivuko vya Kigamboni na Kigongo Busisi ulifungwa na
Kampuni ya Africom Tanzania ambaye Mkurugenzi Mtendaji wake Juma Rajabu
alisema watahakikisha wanafunga mifumo ambayo itadhibiti upotevu wa
mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi ambao ndiyo watumiaji.VICTOR
SIMON
Post a Comment