0
KAMATI BUNGE YA SHAURI
..Mwaandishi wetu

Kamati  bunge ya  kudumu ya serikali za mitaa na tawala za mikoa imezitaka halmsahuri zote nchini kuanzisha kikundi kazi maalumu cha kufanya utafiti, kupitia,kuhakiki na kufanyia tathimini vyanzo vya  mapato ili kubaini mianya ya uvujaji  na mamna ya kuvithibiti na kubuni nyanzo vipya  vya mapato.

Agizo hilo limetolewa na kamati hiyo baada ya kutembelea  kwenye wilaya tatu za mkoa wa Lindi ambazo  ni Lindi manispaa, Nachingwea, na Kilwa  na kubaini kuwepo kwa tatizo la ukusanyaji mapato usioridhisha kutokana na  kuwepo kwa mianya ya ukwepaji wa kodi.
Mwenyekiti wa kamati hiyo DK  Hamisi Kigwangala alisema ukusanyaji wa mapato  katika  halmashauri zilizotembelewa mkoani humo  kutoridhisha,kwa sababu  mbalimbali  ikiwemo  mianya ya ukwepaji kodi  udhamini mdogo wa ukusanyaji wa mapato pamoja na vitendea kazi vya kisasa.
DK,Kigwangala alisema ilikuendana na hali ya mapato ya nchi ni vema serikali ipunguze matumizi yasiyo ya lazima ikiwamo semina,magari ya gharama kubwa(mashangingi) na ukubwa wa baraza la mawaziri(serikali).
Alisema matumizi yanayotumika kwa mambohayo hazina tija wala faida kwa nchi ambayo uchumi wake ni mdogo na wananchi wanahitaji huduma za msingi ikiwamo miradi mbalimbali ya maendeleo.
Wakati huohuo mwenyekiti huyo kwa niaba ya kamati ameitaka serikali kupunguza utegemezi kwa wafadhili na wahisani wa maendeleo badala yake itumie mapato yake yandani  yatakayo na ukusanyaji  na usimamizi  mzuri  wa matumizi  ikiwwezekana  na mwaka huuu serikali  itangaze  kutotegemea  fedha  za ufadhili katika  kutekeleza shughuli  zake  za  maendeleo  badala yake fedha za nje ziwe  za mikopo wenye masharti nafuuu alisema Kigwangala .
Alibainisha kuwa utegemeze  wa fedha za  wafadhili ndio  unaosababisha serikali  kutopeleka fedha  katika halmashauri  kwa wakati ,hivyo  miradi  mingi ya maendeleo  kushindwa  kutekelezwa na  minginne kutomalizika kwa wakati
Sambamba na ushauri na agizo hilo Kigwangala kwaniaba ya kamati hiyo amezitaka halmashauri zote nchini kuunda vikosi kazi vitakafuatilia na kubaini vyanzo vyamapato na mianya inayozikosesha mapato ya ndani halmashauri.Alisema uwezo wa halmashauri kukusanya mapato yake ya ndani hauridhishi hivyo kusababisha mzigo mkubwa wa kuwahudumia wananchi kubebwa na serikali kuu.
Alisema ilikuhakikisha zoezi linafanikiwa wakuu wawilanye kamati hiyo kabla bunge la sasa kuvun.BOFYA HAPA

Post a Comment

 
Top