Naibu
Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mbunge wa Bumbuli na Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Habari na Masoko ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
ambaye hivi karibuni pia ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa January Makamba
---
Na Mwandishi Wetu, Dar
Mbunge
wa Bumbuli na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Habari na Masoko ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambaye hivi karibuni pia ametangaza
nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
January Makamba hivi karibuni ameainisha adhma yake ya kuinua kiwango
cha michezo nchini.
Kwenye
kitabu hicho, Makamba amejibu swali kwamba kitu gani kifanyike ili
Watanzania waweze kujivunia wanamichezo wao. Makamba alisema,
“Inafedhehesha sana kuona kwamba asilimia 79 ya Watanzania walikuwa
hawajazaliwa mara ya mwisho tumeshiriki katika fainali za kombe la
mataifa ya Afrika.
Mwaka
huo huo wa 1980 ndio mara ya kwanza na ya mwisho tuliweza kushinda
medali za Olimpiki. Rafiki yangu Mzee Suleiman Nyambui na Mzee wetu
Filbert Bayi ndio walitutoa kimasomaso kipindi kile. Ni muhimu
kurekebisha hili.”
Ni
ukweli usiopingika kwamba Tanzania imekuwa kama kichwa cha mwendawazimu
katika medani ya kimataifa huku tasnia ya michezo ikiendelea kugubikwa
na migogoro isiyokwisha. Kutokana na migogoro hii, Tanzania inaendelea
kupoteza matumaini ya kung’aa katika medani za kimataifa.
Katika
mazungumzo hayo na Padre Karugendo, Makamba alinukuliwa akisema,
“Lazima tutambue kwamba maendeleo ya michezo yanatokana na vitu muhimu
vitatu. Kwanza, ni lazima kuwepo na vipaji, bahati nzuri nchi yetu ina
vipaji vya kutosha katika aina zote za michezo. Pili, ni miundombinu na
mfumo wa kubaini na kuviendeleza vipaji hivyo, hii bado ni changamoto .
Tatu, ni utawala, uongozi, na uendeshaji wa tasnia ya michezo, hii pia
ni changamoto. Hivi vitu vitatu ni lazima viwepo ili tuweze kupata
mafanikio kwenye medani ya michezo.”
Kama
mgombea wa kwanza kutangaza nia yake ya kugombea nafasi ya Urais katika
uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, Makamba anaungwa mkono na vijana
wengi kutokana na kuendesha siasa zake kisasa, kibunifu na kuepuka
malumbano ya jukwaani.
Katika
mazungumzo hayo Makamba alielezea fikra zake alizonazo hasa hasa kwenye
kuendeleza vipaji vya Watanzania ambapo alisema, “Ni lazima tuanzishe
vituo vikubwa vya michezo au ‘sports academies’ kwenye kila kanda ya
nchi yetu vyenye hadhi ya Kiolimpiki.”
Makamba
aliongeza kwamba, “Kutakuwa na vituo sita vya aina hii katika nchi
yetu ambavyo vitazungukwa na shule za msingi na sekondari za ‘boarding’.
Vituo hivi vitakuwa na lengo la kukusanya wanafunzi wote kwenye kanda
husika ambao wameonekana kuonyesha vipaji ambavyo vinapaswa kuendelezwa.
Ukweli ni kwamba bila kuendeleza vipaji katika mazingira mazuri, basi
tusahau kabisa kufanya vizuri kwenye michezo. Hili linaweza kufanywa kwa
ushirikiano wa serikali na sekta binafsi”.
Mheshimiwa
January Makamba anakuwa mgombea wa kwanza wa Urais kuweka bayana
mipango yake ya Tanzania Mpya katika maandishi. Anaendelea kufunguka
kwamba katika tasnia ya michezo ni muhimu sana kuwekeza katika watoto.
Zaidi ya hapo, kila timu ya ligi kuu ni lazima iwe na akademi na TFF
iendeshe ligi kuu ya timu za watoto.
“Tufikie
wakati ambapo timu za taifa za miaka 10 ijayo ziwe zinaandaliwa kuanzia
sasa, na serikali itenge bajeti kila mwaka kwa timu hizo ili
kuziwezesha kukaa kambini, kufanya mechi za majaribio na kuziwezesha
kushiriki kikamilifu katika mashindano ya kimataifa. Mimi sio muumini wa
hizi kamati za zimamoto kusaidia timu ishinde ghafla ghafla wakati siku
zote watu hawafanyi maandalizi ya muda mrefu” alimalizia Makamba.
Makamba
pia aligusia kuhusu suala la ukata na ufinyu wa bajeti unaokabili
tasnia za michezo. Siku zote tunaona timu za taifa za olimpiki au
jumuiya ya madola kukosa fedha za kukaa kambini ambapo huchangia katika
matokeo hafifu.
“Huko
nyuma, taasisi na mashirika ya umma yalikuwa na timu za michezo
zilizokuwa zinafanya vizuri na kutoa michango kwenye maendeleo ya
michezo. Kwa mfano, Pamba ya Mwanza, Sigara, Reli ya Morogoro, ushiriki
huu ulichangamsha sana michezo na ni lazima turudishe utamaduni huu,”
alimalizia Makamba.
Post a Comment