Katibu mkuu wa ACT-TANZANIA ndugu SAMSON MWIGAMBA akizungumza na wanahabari mapema leo jijini dar es salaam kuhusu maamuzi ya mkutano mkuu wa chama hicho na yanayoendelea ndani ya chama hicho |
NA KAROLI VINSENT
KATIBU mkuu wa Chama cha kipya cha Siasa cha Alliance for
change and Transparency ACT-Tanzania Samson Mwigamba amejikuta akijutia
uamuzi wake,baada ya kusema ni bora angebaki Chama cha Demokrasia na
Mandeleo Chadema kuliko chama alichokuwepo sasa cha ACT-Tanzania
kutokana na kuwepo kwa viongozi wenye ufinyu wa mawazo.
Samson Mwigamba ambaye alifukuzwa Chadema kutokana na kuandaa
mipango ya kuundoa uongozi ulioijenga Chadema Kimafinikio chini ya
Freeman Mbowe, na kukimbilia chama Cha ACT-Tanzania ambapo sasa
kumeibuka mgomgoro wa Uongozi ndani ya Chama hicho.
Kauli hiyo ya imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu
Mkuu huyo wa Chama cha ACT-Tanzania Samson Mwigamba wakati wa Mkutano na
Waandishi wa Habari ambapo amesema ni bora angebaki kwa kamanda wa anga ambako ni Chadema kuliko wapambanaji wa ardhini ambao ni viongozi wa chama hicho kichanga cha siasa cha ACT-Tanzania.
Mwigamba aliongeza kuwa kitendo cha Mwenyekiti wa mda wa
ACT-Tanzania Kadawi Limbu kuitisha mkutano mkuu ambao tayari uliokuwa na
mapungufu kikatiba na kuwatimua Viongozi mbalimbali ambao yeye akiwemo
amesema ni ishara tosha ya kiongozi huyo kuwa kigegeu na mwenye kuwa
na kila ishara ya kutumika .
Shaban Mambo makamu mwenyekiti bara akizungumza |
“Maamuzi yaliyofanywa na Ndugu Limbu hayana uhalali wa kisiasa
,kikatiba na sheria na yalilenga kuwasaidia baadhi ya ,mahasimu wa
kisiasa wa ACT-Tanzania kuonyesha kwamba mimi na wenzangu tuliofukuzwa
chadema ni watu wakorofi na kwamba ilikuwa sahihi kwa Chadema kuchukua
hatua wakati tulikuwa tunadai haki na usawa”alisema Mwigamba
Mwigamba alibainisha kuwa kitendo cha Mwenyekiti Limbu
kumwandikia Msajili wa Vyma vya Siasa nchini kumuomba uchaguzi wa ndani
kwenye chama hicho ufanyika mwakani 2016 ni ishara ya kiongozi huyo
anaogopa uchaguzi ndani ya c hama na pia alivunja katiba ya namba 5 ya
msajili wa vyama vya siasa.
“Sheria za msajili ziko wazi nashangaa huyo mwenyekiti limbu
anazivunja ikiwemo sheria namba 5 ya msajili wa vyama vya siasa nchini
inasema “Uongozi wa muda utabaki na uhalali wake kwa muda ya miezi 12
tangu kupata usajili wa kudumu kama unavyoeleza na sheria za vyama vya
siasa,nashangaa sasa huyu mwenyekiti wa mda anafanya utoto huu wa
kuongeza tena miezi 12 mengine ambayo ni kinyume na taratibu”aliongeza
Mwigamba.
Mwanasheria wa chama hicho THOMAS MATATIZO akisoma maazimio ya chama juu ya viongozi waliovunja taratibu |
Maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Chama hicho.
Akisoma maazimio ya Mkutano mkuu uliofanyika mapema wiki hii
Jijini Dar ES Salaam na kuhudhuliwa na wajumbe 11 kati ya 22.
Akisoma
Maazimo ya Mkutano Mkuu wa Chama hicho kuhusu Viongozi hao walidiriki
kuwafuza viongozi mbalimbali mbali wa chama hicho,Mwanasheria wa chama
hicho THOMAS MATATIZO alisema Mkutano huo mkuu umefikia hatua ya
kumwondo mwenyekiti wa ACT-Tanzania Kadawi Limbu ambaye amevunja kanuni
na sheria ya chama hicho.
Wanahabari kazini |
“Kwa
kuzingatia mamlaka yake ya kikatiba (Ibara ya katiba 27 (c),kamati kuu
imemsimamisha ndugu Kadawi limbu, huku Naibu Katibu mkuu bara Leopold
Mahona atachukuliwa hatua kwenye mkutano mkuu wa Halmashauri kuu ambao ndiowenye mamlaka ya uteuzi wake”aliileza Mwanasheria huyo
Post a Comment